Zaburi
1
Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha. Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku. Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa. Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hivyo waovu hawatasimama katika hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.