2
Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
3 wazao wa Paroshi | 2,172 |
4 wazao wa Shefatia | 372 |
5 wazao wa Ara | 775 |
6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) | 2,812 |
7 wazao wa Elamu | 1,254 |
8 wazao wa Zatu | 945 |
9 wazao wa Zakai | 760 |
10 wazao wa Bani | 642 |
11 wazao wa Bebai | 623 |
12 wazao wa Azgadi | 1,222 |
13 wazao wa Adonikamu | 666 |
14 wazao wa Bigwai | 2,056 |
15 wazao wa Adini | 454 |
16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) | 98 |
17 wazao wa Besai | 323 |
18 wazao wa Yora | 112 |
19 wazao wa Hashumu | 223 |
20 wazao wa Gibari | 95 |
21 watu wa Bethlehemu | 123 |
22 watu wa Netofa | 56 |
23 watu wa Anathothi | 128 |
24 watu wa Azmawethi | 42 |
25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi | 743 |
26 wazao wa Rama na Geba | 621 |
27 watu wa Mikmashi | 122 |
28 watu wa Betheli na Ai | 223 |
29 wazao wa Nebo | 52 |
30 wazao wa Magbishi | 156 |
31 wazao wa Elamu ile ingine | 1,254 |
32 wazao wa Harimu | 320 |
33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono | 725 |
34 wazao wa Yeriko | 345 |
35 wazao wa Senaa | 3,630 |
36 Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) | 973 |
37 wazao wa Imeri | 1,052 |
38 wazao wa Pashuri | 1,247 |
39 wazao wa Harimu | 1,017 |
40 Walawi:
wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) | 74 |
41 Waimbaji:
42 Mabawabu wa lango la Hekalu:
wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai | 139 |
43 Watumishi wa Hekalu:
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49 wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54 wazao wa Nesia na Hatifa.
55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
58 Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni | 392 |
59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
60 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda | 652 |
61 Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.
66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
67 ngamia 435 na punda 6,720.
68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.
69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.