Zaburi 117
Sifa za Mwenyezi Mungu
Msifuni Mwenyezi Mungu, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa Mwenyezi Mungu unadumu milele.
 
Msifuni Mwenyezi Mungu.*
* Zaburi 117:2 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.