13
1 Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaeni( ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli.
2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, “Niteengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia.”
3 Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende.
4 Kwa hiyo Barnabas na Sauli walimtii Roho Mtakatifu na walitelemka kuelekea Seleukia; Kutoka huko walisafiri baharini kuelekea kisiwa cha Kipro.
5 Walipokuwa katika mji wa Salami, walilitangaza neno la Mungu katika Masinagogi ya Wayahudi. Pia walikuwa pamoja na Yohana Marko kama msaidizi wao.
6 Walipokwenda katika kisiwa chote mpaka Pafo, walikuta mtu fulani mchawi, Myahudi nabii wa uongo, ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu.
7 Mchawi huyu alishirikiana na Liwali Sergio Paulus, aliyekuwa mtu mwenye akili. Mtu huyu aliwaalika Barnaba na Sauli, kwa sababu alihitaji kusikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima “yule mchawi” (hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa) aliwapinga; alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani.
9 Lakini Sauli aliyeitwa Paulo, alikuwa amejazwa na Roho Mtakatikfu, akamkazia macho
10 na akasema “Ewe mwana wa Ibilisi, umejazwa na aina zote za udanganyifu na udhaifu. Wewe ni adui wa kila aina ya haki. Hautakoma kuzigeuza njia za Bwana, zilizonyooka, je utaweza?
11 Sasa tazama, mkono wa Bwana upo juu yako, na utakuwa kipofu. Hautaliona Jua kwa muda” mara moja ukungu na giza vilianguka juu ya Elimas; alianza kuzunguka pale akiomba watu wamwongoze kwa kumshika mkono.
12 Baada ya liwali kuona kilichotokea, aliamini, kwa sababu alishangazwa kwa mafundisho kuhusu Bwana.
13 Sasa Paulo na rafiki zake walisafiri majini kutoka Pafo na wakafika Perge katika Pamfilia. Lakini Yohana aliwaacha na kurudi Yerusalemu.
14 Paulo na rafiki yake walisafiri kutoka Perge na wakafika Antiokia ya Pisidia. Huko walikwenda katika sinagogi siku ya Sabato na kukaa chini.
15 Baada ya kusoma sheria na manabii, viongozi wa sinagogi aliwatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mnao ujumbe wa kutia moyo watu hapa, semeni”
16 Kwa hiyo Paulo alisimama na kuwapungia mkono; alisema, “Wanaume wa Israeli na enyi mnao mtii Mungu, sikilizeni.
17 Mungu wa hawa watu wa Israeli aliwachagua baba zetu na kuwafanya watu wengi walipokaa katika nchi Misri, na kwa mkono wake kuinuliwa aliwaongoza nje yake.
18 Kwa miaka arobaini aliwavumilia katika jangwa.
19 Baada ya kuyaharibu mataifa saba katika nchi ya Kaanani, aliwapa watu wetu nchi yao kwa urithi.
20 Matukio haya yote yalitokea zaidi ya miaka mia nne na hamsini. Baada ya vitu hivi vyote, Mungu aliwapa waamuzi mpaka Samweli Nabii.
21 Baada ya haya, watu waliomba mfalme, hivyo Mungu aliwapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila la Benjamini, kuwa mfalme kwa miaka arobaini.
22 Kisha baada ya Mungu kumuondoa katika ufalme, alimwinua Daudi kuwa mfalme wao. Ilikuwa ni kuhusu Daudi kwamba Mungu alisema, 'Nimempata Daudi mwana wa Yese kuwa mtu apendezwaye na moyo wangu; ambaye atafanya kila kitu nipendacho.'
23 Kutoka kwenye ukoo wa mtu huyu Mungu ameiletea Israeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi kufanya.
24 Hili lilianza kutokea, kabla ya Yesu kuja, Yohana kwanza alitangaza ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli.
25 Naye Yohana alipokuwa akimalizia kazi yake, alisema, 'Mwanifikiri mimi ni nani? mimi si yule. Lakini sikilizeni, ajaye nyuma yangu, sisitahili kulegeza viatu vya miguu yake.'
26 Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu, ni kwa ajili yetu kwamba ujumbe huu wa ukombozi umetumwa.
27 Kwa wale waishio Yerusalemu, na watawala wao, hawakumtambua kwa uhalisia, na wala hawakuutambua ujumbe wa manabii ambao husomwa kila Sabato; kwa hiyo walitimiliza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu kifo Yesu.
28 Japokuwa hawakupata sababu nzuri kwa kifo ndani yake, walimwomba Pilato amuue.
29 Walipomaliza mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye, walimshusha kutoka mtini na kumlaza kaburini.
30 Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu.
31 Alionekana kwa siku nyingi kwa wale waliokwenda pamoja naye kutoka Galilaya kuelekea Yerusalemu. Watu hawa sasa ni mashahidi wa watu.
32 Hivyo tunawaletea habari njema kuhusu ahadi walizopewa mababu zetu.
33 Mungu aliweka ahadi hizi kwetu, watoto wao, katika hilo alimfufua Yesu na kumrudisha tena katika uhai. Hili pia liliandikwa katika Zaburi ya pili: 'Wewe ni Mwanangu, leo nimekuwa Baba yako'
34 Pia kuhusu ukweli ni kwamba alimfufua kutoka wafu ili kwamba mwili wake usiharibike, ameongea hivi: 'Nitakupatia utakatifu na baraka halisi za Daudi'
35 Hii ndiyo sababu kasema pia katika zaburi nyingine, 'Hautaruhusu mtakatifu wako kuuona uozo.'
36 Kwa kuwa baada ya Daudi kutumikia mapenzi ya Mungu katika kizazi chake, alilala, alilazwa pamoja na baba zake, na aliuona uaharibifu,
37 Lakini aliyefufuliwa na Mungu hakuuona uharibifu.
38 Hivyo na ifahamike kwenu, ndugu, kupitia mtu huyu, msamaha wa dhambi umehubiriwa.
39 Kwa yeye kila aaminiye anahesabiwa haki na mambo yote ambayo sheria ya Musa isingewapatia haki.
40 Hivyo basi kuweni waangalifu kwamba kitu walichokiongelea manabii kisitokee kwenu:
41 'Tazama, enyi mnaodharau, na mkashangae na mkaangamie; kwa vile nafanya kazi katika siku zenu, Kazi ambayo hamwezi kuiamini, hata kama mtu atawaeleza.”
42 Wakati Paulo na Barnaba walipoondoka, watu wakawaomba waongee maneno haya siku ya Sabato ijayo.
43 Wakati mkutano wa sinagogi ulipokwisha, Wayahudi wengi na waongofu thabiti waliwafuata Paulo na Barnaba, ambao waliongea nao na waliwahimiza waendelee katika neema ya Mungu.
44 Sabato iliyofuata, karibu mji mzima ulikusanyika kusikia neno la Mungu.
45 Wayahudi walipoona makutano, walijawa na wivu na kuongea maneno yaliyopinga vitu vilivyosemwa na Paulo na walimtukana.
46 Lakini Paulo na Barnaba waliongea kwa ujasiri na kusema, “Ilikuwa ni muhimu kwamba neno la Mungu liongelewe kwanza kwenu. Kwa kuwa mnalisukumia mbali kutoka kwenu nakujiona kuwa hamkusitahili uzima wa milele, angalieni tutawageukia Mataifa.
47 Kama ambavyo Bwana ametuamuru, akisema, 'Nimewaweka ninyi kama nuru kwa watu wa mataifa, kwamba mlete wokovu kwa pande zote za dunia.”
48 Mataifa waliposikia hili, walifurahi na kulisifu neno la Bwana. Wengi waliochaguliwa kwa uzima wa milele waliamini.
49 Neno la Bwana lilienea nchi yote.
50 Lakini wayahudi waliwasihi waliojitoa na wanawake muhimu, pia na viongozi wa mji. Haya yalichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na waliwatupa nje ya mipaka ya mji.
51 Lakini Paulo na Barnaba walikung'uta vumbi ya miguu yao. Kisha walienda kwenye mji wa Ikonia.
52 Na wanafunzi walijawa na furaha pamoja na Roho mtakatifu.