6
1 Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na kwa wale ambao wameokoka katika nchi ya mlima wa Samaria, watu mashuhuri bora wa mataifa, ambao nyumba ya Israeli huja kwa ajili ya msaada!
2 Viongozi wenu husema, “Pita kwenda Kalne na mkatazame; kutoka huko nendeni hadi Hamathi, mji mkubwa; kisha nendeni chini hata Gathi ya Wapelestina. Je ni wabora kuliko falme zenu mbili? Je kuna mpaka mkubwa kuliko mpaka wenu?”
3 Ole wao wale waiwekao siku ya majanga na kufanya ufalme kuwa kinyume kusogea karibu.
4 Wamelala juu ya vitanda vya pembe na kupumzika juu ya viti vyao. Wakala wana kondoo kutoka kwenye kundi na ndama kutoka kwenye zizi.
5 Wanaimba nyimbo za kijinga kwenye muziki wa kinubi; wanatunga kwenye vyombo kama vya Daudi.
6 Wanakunywa mvinyo kutoka kwenye bakuli na kujipaka mafuta wenyewe kwa mafuta ya marahamu, lakini hawahuzuniki juu ya mateso ya Yusufu.
7 Hivyo sasa watakwenda utumwani pamoja na watumwa wakwanza, na kelele za hao waliojinyoosha zitapita.
8 “Mimi Bwana Yahwe, nimeapa kwa nafsi yangu -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, naizira fahari ya Yakobo; nachukia boma zake. Kwa hiyo nitautoa huo mji pamoja vyote vilivyomo humo.”
9 Itakuja kuhusu kwamba kama kuna wanaume kumi waliobakia kwenye nyumba moja, watakufa.
10 Wakati ndugu wa mtu huyo atakapokuja kuchukua miili yao-yule ambaye awachomaye baada ya kuleta maiti katika nyumba-kama akisema kwa mtu katika nyumba, “Je kuna mtu yuko pamoja nawe?” Vipi kama yule akisema, “Hapana.” Kisha atasema, “Kaa kimya, kwa kuwa hatulitaja jina la Yahwe.”
11 Tazama, Yahwe atatoa amri, na nyumba kubwa itapigwa kuwa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa na nyufa.
12 Je farasi watakimbia juu ya mteremko wa miamba? Je mtu atalima huko na ng'ome? Bado mmegeuza haki kuwa sumu na tunda la haki kuwa uchungu.
13 Ninyi mnaofurahia juu ya Lo Debari, msemao, “Je hatukuchukua Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”
14 Lakini tazama, nitainua juu yenu taifa, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe, Mungu wa majeshi. Watawatesa ninyi kutoka Lebo Hamathi hata kijito cha Araba.”