11
1 Nahisi kwamba mngevumiliana na mimi katika baadhi ya upumbavu. Lakini kwa kweli mnavumiliana na mimi.
2 Kwa kuwa ni mwenye wivu kuhusu ninyi. Nina wivu wa Mungu kwa ajili yenu, tangu nilipowaahidi ninyi kwenye ndoa ya mume mmoja. Niliahidi kuwaleta ninyi kwa Kristo kama bikra safi.
3 Lakini ninaogopa kwamba kwa namna fulani, kama nyoka alivyomdanganya Eva kwa hila yake, mawazo yenu yanaweza kupotoshwa mbali kutoka kwenye ibada halisi na safi kwa Kristo.
4 Kwa kuwa kwa mfano kwamba mtu fulani akaja na kutangaza Yesu mwingine tofauti na yule tuliyewahubiri. Au kwa mfano kwamba mkapokea roho mwingine tofauti na yule mliyempokea. Au kwa mfano kwamba mkapokea injili nyingine tofauti na ile mliyoipokea. Mkavumilia mambo haya vema inatosha!
5 Kwa kuwa nadhani kwamba mimi si miongoni mwa walio duni kwa hao wanaoitwa mitume-bora.
6 Lakini hata kama mimi sijafundishwa katika kutoa hotuba, siko hivyo katika maarifa. Kwa kila namna na katika mambo yote tumelifanya hili kujulikana kwenu.
7 Je, nilifanya dhambi kwa kujinyenyekeza mwenyewe ili ninyi muweze kuinuliwa? Kwa kuwa nilihubiri kwa uhuru injili ya Mungu kwenu.
8 Nilinyang'anya makanisa mengine kwa kupokea msaada kutoka kwao ili kwamba ningeweza kuwahudumia ninyi.
9 Wakati nilipokuwa nanyi na nilikuwa katika uhitaji, sikumlemea yeyote. Kwa kuwa mahitaji yangu yalitoshelezwa na ndugu waliokuja kutoka Makedonia. Katika kila kitu nimejizuia mwenyewe kutokuwa mzigo kwenu, na nitaendelea kufanya hivyo.
10 Kama kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, huku kujisifu kwangu, hakutanyamazishwa katika sehemu za Akaya.
11 Kwa nini? Kwa sababu siwapendi? Mungu anajua nawapenda.
12 Lakini kile ninachokifanya, nitakifanya pia. Nitakifanya ili kwamba niweze kuzuia nafasi ya wale wanaotamani nafasi ya kuwa kama tulivyo katika kile kile wanachojivunia.
13 Kwa kuwa watu wale ni mitume wa uongo na watendakazi wadanganyifu. Wanajigeuza wenyewe kama mitume wa Kristo.
14 Na hii haishangazi, kwa kuwa hata Shetani hujigeuza mwenyewe kama malaika wa nuru.
15 Hii haina mshangao mkubwa kama watumishi wake pia kujigeuza wenyewe kama watumishi wa haki. Hatma yao itakuwa kama matendo yao yastahilivyo.
16 Nasema tena: Basi na asiwepo mtu yeyote anayefikiri mimi ni mpumbavu. Lakini kama mkifanya, nipokeeni mimi kama mpumbavu ili niweze kujisifu kidogo.
17 Kile ninachosema kuhusu huku kujiamini kwa kujivuna hakuhukumiwi na Bwana, lakini nazungumza kama mpumbavu.
18 Kwa vile watu wengi hujivuna kwa jinsi ya mwili, nitajivuna pia.
19 Kwa kuwa mlichukuliana kwa furaha na wapumbavu, ninyi wenyewe mna busara!
20 Kwa kuwa mnachukuliana na mtu kama akikutia utumwani, kama husababisha mgawanyiko kati yenu, kama akiwatumia ninyi kwa faida yake, kama akijiweka juu hewani, au kama akiwapiga usoni.
21 Nitasema kwa aibu yetu kwamba sisi tukuwa dhaifu sana kufanya hivyo. Na bado kama yeyote akijivuna— nazungumza kama mpumbavu— mimi pia nitajivuna.
22 Je, wao ni Wayahudi? Na mimi ni hivyo. Je, wao ni Waisraeli? Na mimi ni hivyo. Je, wao ni uzao wa Abrahamu? Na mimi ni hivyo.
23 Je, wao ni watumishi wa Kristo? {Nanena kama nilirukwa na akili zangu. } Mimi ni zaidi. Nimekuwa hata katika kazi ngumu zaidi, mbali zaidi ya kuwa vifungoni, katika kupigwa kupita vipimo, katika kukabili hatari nyingi za kifo.
24 Kutoka kwa Wayahudi nimepokea mara tano “mapigo arobaini kutoa moja.”
25 Mara tatu nilipigwa kwa fimbo. Mara moja nilipigwa mawe. Mara tatu nilinusurika melini. Nimetumia usiku na mchana katika bahari wazi.
26 Nimekuwa katika safari za mara kwa mara, katika hatari za mito, katika hatari za majambazi, katika hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, katika hatari kutoka kwa watu wa mataifa, katika hatari ya mji, katika hatari ya jangwa, katika hatari ya bahari, katika hatari kutoka kwa ndugu waongo.
27 Nimekuwa katika kazi ngumu na katika maisha magumu, katika usiku mwingi wa kutolala, katika njaa na kiu, mara nyingi katika kufunga, katika baridi na uchi.
28 Mbali na kila kitu kingine, kuna msukumo wa kila siku juu yangu wa wasiwasi wangu kwa ajili ya makanisa.
29 Nani ni dhaifu, na mimi siyo dhaifu? Nani amesababisha mwingine kuanguka dhambini, na mimi siungui ndani?
30 Kama ni lazima nijivune, nitajivunia kuhusu kile kinachoonyesha udhaifu wangu.
31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye anatukuzwa milele, anajua kwamba mimi sidanganyi.
32 Kule Dameski, mkuu wa mkoa chini ya mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Dameski ili kunikamata.
33 Lakini niliwekwa kikapuni, kupitia dirishani katika ukuta, na nikanusurika kutoka mikononi mwake.