13
1 Hii ni mara ya tatu kwamba nakuja kwenu. “Kila shitaka lazima lijengwe na uthibitisho wa mashahidi wawili au watatu.”
2 Nimekwishashasema kwa hao waliotenda dhambi kabla na kwa wengine wote wakati nilipokuwa huko mara ya pili, na ninasema tena: Nitakapokuja tena, sitawavumilia.
3 Nawaambia ninyi hili kwa sababu mnatafuta ushahidi kwamba Kristo ananena kupitia mimi. Yeye sio dhaifu kwenu, badala yake, yeye ni mwenye nguvu ndani yenu.
4 Kwa kuwa alisulibiwa katika udhaifu, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Kwa kuwa sisi pia tu dhaifu ndani yake, lakini tutaishi naye kwa nguvu za Mungu miongoni mwenu.
5 Jichunguzeni wenyewe muone kama mko katika imani. Jipimeni wenyewe. Hamgundui kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Yeye yumo, vinginevyo kama hamjathibitishwa.
6 Na nina ujasiri kwamba ninyi mtagundua kwamba sisi hatukukataliwa.
7 Sasa tunaomba kwa Mungu kwamba msiweze kufanya chochote kibaya. Siombi kwamba sisi tuweze kuonekana tumepita jaribu, badala yake ninaomba kwamba muweze kufanya kilicho sahihi, Ingawa tunaweza kuonekana tumeshindwa jaribu.
8 Kwa kuwa sisi hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, lakini ni kwa ajili ya kweli tu.
9 Kwa kuwa tunafurahi wakati tunapokuwa dhaifu nanyi mkiwa na nguvu. Tunaomba pia kwamba muweze kufanywa wakamilifu.
10 Nayaandika mambo haya wakati nikiwa mbali nanyi, ili kwamba wakati nikiwa pamoja nanyi sihitaji kuwaonesha ukali ninyi. Sihitaji kutumia mamlaka Bwana aliyonipaa mimi niwajenge na siyo kuwaharibu chini.
11 Hatimaye, ndugu wa kiume na wa kike, furahini! fanyeni kazi kwa ajili ya urejesho, mtiwe moyo, kubalianeni ninyi kwa ninyi, muishi katika amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
12 Salimianeni kila mmoja kwa busu takatifu.
13 Waumini wote wanawasalimu.
14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja nanyi nyote.