25
1 Iwapo kutakuwa na malumbano kati ya wanaume na wakaenda mahakamani, na waamuzi wakawahukumu, basi watamwachilia mtakatifu na kumhukumu muovu.
2 Iwapo mwanamume mwenye hatia anastahili kupigwa, basi muamuzi atamfanya alale chini na kupigwa mbele zake kwa idadi iliyoamriwa kulingana na kosa lake.
3 Muamuzi anaweza kumpatia mapigo arobaini, lakini hapaswi kuvuka idadi hiyo; kwa maana akivuka idadi hiyo na kumpiga kwa mapigo mengi zaidi, basi Muisraeli mwenzako atakuwa kaaibishwa mbele ya macho yenu.
4 Haupaswi kumfunga punda wako pua na mdomo anapokuwa akilima shamba lako.
5 Iwapo kaka wanaishi pamoja na mmoja wao akafariki bila kuwa na mwana, basi mke wa marehemu hatakiwi kuolewa na mtu nje ya familia. Badala yake, kaka yake mumewe anapaswa kulala naye na kumchukua kuwa mke wake na kutekeleza wajibu wa kaka wa mume kwake.
6 Hii ni kwamba mtoto wa kwanza atakayezaliwa arithi chini ya jina la kaka yake mwanamume aliyefariki, ili jina lake lisiangamie ndani ya Israeli.
7 Lakini kama mwanamume hataki kumchukua mke wa kaka yake awe wake, basi mke wa kaka yake anapaswa kwenda malangoni mpaka kwa wazee na kusema, “Kaka wa mume wangu amekataa kuwajibika kwa niaba ya jina la kaka yake humu Israeli; hataki kufanya wajibu wa kaka wa mume kwangu”.
8 Kisha wazee wa mji wake wanapaswa kumuita na kuzungumza naye. Lakini tuseme atasisitiza na kusema, “Sitaki kumchukua”.
9 Basi mke wa kaka yake anatakiwa kuja kwake mbele ya wazee, kumvua ndara zake miguuni mwake, na kumtemea usoni. Anapaswa kumjibu na kusema, “Hivi ndivyo kinachofanyika kwa mwanamume asiyetaka kujenga nyumba ya kaka yake”.
10 Jina lake Israeli litaitwa, “Nyumba ya mtu aliyevuliwa ndara zake”.
11 Iwapo wanamume wamepigana wao kwa wao, na mke wa mmoja wao kaja kumkomboa mumewe dhidi ya yule aliyempiga, naye akanyosha mkono wake na kumshika sehemu za siri,
12 basi unapaswa kuukata mkono yake; jicho lako halipaswi kuwa na huruma.
13 Haupaswi kuwa na mizani ya uzito tofauti katika mfuko wako, mkubwa na mdogo.
14 Hautakiwi kuwa na vipimo tofauti ndani ya nyumba yako, vikubwa na vidogo.
15 Unatakiwa kuwa na uzito kamili na wa haki; unatakiwa kuwa na vipimo kamili na vya haki, ili siku zako ziwe ndefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia.
16 Kwa maana wote wanaofanya vitu hivi, wote wanaovunja haki, ni chukizo kwa Yahwe Mungu wako.
17 Kumbuka ni jambo gani Amaleki alichofanya kwako barabarani ulipokuwa ukitoka Misri,
18 jinsi alivyokutana na wewe barabarani na kuwashambulia kati yenu kwa nyuma, wale waliokuwa wamelegea nyuma, mlipokuwa dhaifu na kuchoka, hakumheshimu Mungu.
19 Kwa hiyo, Yahwe Mungu wako atakapowapa pumziko kutoka kwa maadui zako kila sehemu, katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia kumiliki kama urithi, hautakiwi kusahau kuwa unapaswa kufuta kumbukumbu ya Waamaleki chini ya mbingu.