3
1 Kisha tuligeuka na kwenda njia ya juu Bashani. Ogi, mfalme wa Bashani, alikuja na kutuvamia, yeye na watu wake wote, kupigana huko Edrei.
2 Yahwe aliniambia mimi, “Usimuogope; kwa kuwa nimekupa ushindi dhidi yake na nimewaweka watu wake wote na nchi yake chini ya utawala wako. Utamfanya kama ulivyomfanya Sihoni, mfalme wa Amorites, aliyeishi Heshbon.
3 Kwa hiyo Yahwe Mungu wetu pia alitupa ushindi dhidi ya Ogi mfalme wa Bashani, na watu wake wote waliwekwa chini ya utawala wetu. Na tulimpiga mpaka kufa na hakuna yoyote wa watu wake walibaki.
4 Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo; hapakuwa na mji hata mmoja ambao hatukuchukua kutoka kwao: miji sitini - mikoa ya Argobi yote, ufalme wa Ogi Bashani.
5 Hii ilikuwa miji iliyoimarishwa na kuta ndevu, malango, na vizuizi, hii ilikuwa licha ya vijiji vingi sana vilivyokuwa havina kuta.
6 Tuliviangamiza kabisa, kama tulivyofanya kwa Sihoni mfalme wa Heshbon, kabisa tuliangamiza kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo.
7 Lakini ng'ombe wote na mateka ya miji, tilichukua kama mateka wetu.
8 Kwa wakati huo tulichukua nchi kutoka kwenye mkono wa wafalme wawili wa Amorites, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kutoka kwenye bonde la Arnon kwenda mlima wa Hermoni,
9 (Mlima wa Hermoni, Wasidonia huita Sirioni, na Wamorites huita Seniri)
10 na miji yote ya tambarare, yote Gileadi, na yote Bashani kupita njia yote ya Salekah na Edrei, miji ya ufalme wa Ogi huko Bashani”.
11 (Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.)
12 “Hili eneo ambalo tulichukua kumiliki kwa wakati huo-kutoka Aroer, kwamba ni kwa bonde la Arnon, na nusu ya nchi ya mlima wa Gileadi, na miji yake-Nilimpa Reubenites na kwa Gadites.
13 Waliobaki wa Gileadi na Bashani yote, ufalme wa Ogi, Niliwapa nusu kabila la Manasseh: kwa wote wa Argob, na Bashani yote. (Eneo hilo linaitwa nchi ya Refaim)
14 Jair, mzao wa Manasseh, alichukuwa mkoa wote wa Argob, kuelekea mpaka wa Geshunites na wa Maacathites. Aliita mkoa hata Bashani kwa jina lake, Havvothi Jair, hadi leo.)
15 Nilimpa Gileadi kwa Machir.
16 Kwa Reubenites na kwa Gadites nilitoa eneo kutoka kwa Gileadi kuelekea bonde la Arnon- katikati mwa bonde ni mpaka wa eneo- na kuelekea mto wa Jabbok, ambao umepakana ni wazao wa Ammoni.
17 Moja ya mipaka mingine pia ni tambarare ya bonde la mto wa Yordani, kutoka Chinnerethi kuelekea bahari ya Arabah(ambayo ni bahari ya Chumvi) kuelekea miteremko wa mlima wa Pisgah mashariki.
18 Nilikuamuru wewe kwa wakati huo, kusema, Yahwe Mungu wako amekupa nchi hii kuimiliki, wewe, wamaume wote wa vita, watapita wakiwa na silaha mbele ya ndugu zako, watu wa Israeli.
19 Lakini wake zenu, watoto wenu, na ng'ombe zenu (najua ya kuwa una ng'ombe wengi) watabaki katika miji yenu niliyowapa,
20 mpaka Yahwe awape pumziko ndugu zenu, kama alivyo kwenu, mpaka wamiliki pia nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ng'ambo ya pili Yordani, kisha mtageuka, kila mtu wenu, kwa mali zenu ambazo nimekwishawapa.
21 Nilimwamuru Yoshua kwa wakati huo, kusema, 'Macho yenu yameona yote yale Yahwe Mungu wenu amefanya kwa hawa wafalme wawili; Yahwe atafanya hivyo kwa falme zote kote mtakakoenda.
22 Hamtawaogopa, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye atakaoawapigania.'
23 Nilimsihi Yahwe kwa wakati huo, kusema,
24 'O Bwana Yahwe, umeanza kumuonesha mtumwa wako ukuu wako na mkono wako wa hodari; kwa kuwa nani mungu aliyeko huko mbinguni au duniani ambaye anaweza kufanya kazi zilezile kama ilivyofanya, na matendo yaleyale makuu?
25 Hebu niende juu, Ninakuoma, na nione nchi nzuri ambayo ng'ambo ya pili ya Yordani, ile nchi nzuri ya mlima, na pia Lebanoni.
26 Lakini Yahwe alikuwa amenikasirikia mimi kwa sababu yenu, hakunisikiliza mimi. Yahwe alisema kwangu, “Hebu hii iwe ya kutosha kwako - usizungumze zaidi tena kwangu kuhusu jambo hili.
27 nenda juu ya kilele cha Pisgah na uinue macho yako magharibi, mashariki, kusini na mashariki; tazama kwa macho yako kwa kuwa hautaenda zaidi ya Yordani.
28 Badala yake, mwelekeze Yoshua na kumtia moyo na kumuimarisha, kwa kuwa ataenda zaidi mbele ya watu, na atawasababisha kuirithi nchi ambayo mtaiona.
29 Kwa hiyo tulibaki katika bonde mkabala mwa Beth Peor.