10
1 Nilipokuwa nikingalia mbele ya anga ambalo liliyokuwa juu ya vichwa vya kerubi; kitu kikawatokea juu yao kama rangi ya samawati mwonekano wake ulikuwa kama kiti cha enzi.
2 Kisha Yahwe akaongea na yule mtu alikuwa maevaa nguo za kitani na kusema, “Nenda kati ya magurudumu chini ya kerubi, na jaza mikono yako yote na watawanye juu ya mji.” Kisha yule mtu akaenda ndani nikiwa natazama.
3 Kerubi likasimama juu ya upande wa kulia wa nyumba wakati yule mtu alipoingia, na wingu likaja a ndani ya uzio.
4 Utukufu wa Yahwe ukainuka kutoka kwenye kerubi na kusimama kwenye kizingiti cha nyumba. Ukaijaza nyumaba kwa wingu, na uzio ulikuwa umejaa nuru ya utukufu wa Yahwe.
5 Sauti ya mabawa ya kerubi ikasikika kwa mbali nje ya uzio, kama sauti ya Mungu mwenyezi wakati akiwa anaongea.
6 Ikawa kuhusu, Mungu alipoamwamuru yule mtu aliyekuwa amevaa nguo za kitani na kusema, “Chukua moto kutoka kwenye ya kerubi,” yule mtu akaenda na kusimama karibu na gurudumu.
7 Kerubi akaunyoosha mkono wake kwenye kerubi kwenye moto uliokuwa miongoni mwa kerubi, na kuiacha juu na kuiweka kwenye mikono ya yule mtu aliyekuwa amevaa vazi la kitani. Yule mtu akaichukua na kurudi.
8 Nikaona juu ya kerubi kitu kama mkono wa mtu juu ya mabawa yao.
9 Hivyo nikaona, na tazama! Magurudumu manne yalikuwa karibu na kerubi-gurudumu moja karibu na kila kerubi-na mwonekano wa hayo magurudumu ulikuwa kama jiwe la zabarajadi.
10 Mwonekano wake ulikuwa unaofanana kama wa wote wanne, kama gurudumu lililokuwa kwenye gurudumu lingine.
11 wakati walipokuwa wakitembea, walienda katika pande zote nne bila kugeuka katika kwenye njia nyingine. Badala yake, popote kichwa kilipoelekea, walilifuata. Hawakugeuka kwenye njia yeyote nyingine walipokuwa wakienda.
12 Mwili wao wote-pamoja na migongo yao, mikono yao, na mabawa yao-vilikuwa vimefunikwa kwa macho, na macho kufunika magurudumu manne kuzunguka pote pia.
13 Nilikuwa nasikia, magurudumu yalikuwa yakiita, “Kuzunguka.”
14 Walikuwa na nyuso nne kila moja; uso wa kwanza ulikuwa uso wa kerubi, uso wa pili ulikuwa uso wa mtu, uso wa tatu ulikuwa uso wa simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa malaika.
15 Kisha makerubi-hawa walikuwa viumbe hai nilivyokuwa nimeviona karibu na Keberi Kanali-wakainuka juu.
16 Popote makerubi walipoenda, magurudumu yalienda karibu nao, na popote makerubi walipoinua juu mabawa yao kupaa juu kutoka kwenye nchi, magurudumu hayakugeuka. Yaliendelea kuwa karibu nao.
17 Wakati makerubi waliposimama, magurudumu yalisimama pia, na wakati walipoinuka juu, magurudumu yaliinuka juu pamoja nao, kwa kuwa roho wa vile viumbe hai walikuwa kwenye magurudumu.
18 Kisha utukufu wa Yahwe ukaja kutoka juu ya kizingiti cha nyumba na kusimama juu ya kerubi.
19 Lile kerubi likaacha juu mabawa na kuinuka kutoka kwenye jicho langu wakati walipotoka nje, na yale magurudumu yakafanya vivyo hivyo karibu yao. Wakasimama upande wa mashariki kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, na utukufu wa Mungu wa Israeili ukaja juu yao kutoka juu.
20 Hawa walikuwa viumbe hai ambao niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na Kebari Kanali, hivyo nilijua kwamba walikuwa makerubi!
21 Walikuwa na macho manne kila mmoja na mabawa manne, na mfanano wa nyuso zao zilikuwa na mfanano wa mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao,
22 na mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama nyuso nilizokuwa nimeziona kwa maono huko Keberi Kanali, na kila mmoja wao alienda mbele.