16
1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, mwambie Yerusalemu kuhusu machukizo yake,
3 na useme, 'Bwana Yahwe asema hivi kwa Yerusalemu: Mwanzo wako na kuzaliwa kwako kulichukua nafasi katika nchi ya Kanaani; baba yako alikuwa Mwamori, na mama yako alikuwa Mhiti.
4 Katika siku ya kuzaliwa kwako, mama yako hakukata kitovu chako, wala hakukuosha kwenye maji usafishwe au kukuchua kwa chumvi, wala kukusitiri nguo.
5 Hakuna jicho lililokuhurumia kufanya haya mambo kwa ajili yako, kukuhurumia wewe. Katika siku uliyozaliwa, kwa kuchukiwa uhai wako, ulitupwa nje uwandani.
6 Lakini nilipita karibu nawe, nalikuona ukijinyonga kwa damu yako mwenyewe, “kubaki hai!”
7 Nimekufanya ukue kama mmea katika shamba. Umeongezeka na kuwa mkubwa, na umekuwa mzuri wa wazuri. Maziwa yako yakawa thabiti, na nywele zako zikawa nyingi, ingawa ulikuwa uchi huna nguo.
8 Nilipita karibu nawe tena, na nalikuona. Tazama! wakati wa upendo umefika kwako, hivyo nikatandika joho langu juu yako na kufunika uchi wako. Kisha nikaapa kwako na kukuleta kwenye agano-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na ukawa wangu.
9 Basi nilikuosha kwa maji na kukufuta damu yako, na kukupaka mafuta.
10 Nilikuvalisha nguo ya taraza na kukuwekea makuzi ya ngozi kwenye miguu yako. Nilikufungia kwa kitani kizuri na kukufunika kwa hariri.
11 Kisha nalikupamba kwa vito, na kukuvalisha vikuku kwenye mikono yako, na mkufu kwenye shingo yako.
12 Nalitia hazama katika pua yako na hereni katika masikio yako, na taji nzuri juu ya kichwa chako.
13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, na ulivaa kitani safi, hariri, na ngu za taraza; ulikula unga mzuri, asali, na mafuta, na ulikuwa mzuri sana, na ukawa malkia.
14 Umaarufu wako ukaenda miongoni mwa mataifa kwa sababu ya uzuri wako, kwa kuwa ulikuwa mkamili katika ukuu niliokuwa nimekupa-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
15 Lakini ulitumaini uzuri wako, na ukafanya kama kahaba kwa sababu ya umaarufu wako; umeyamwaga matendo yako ya kikahaba kwa kila aliyepita karibu, ili kwamba uzuri wako uwe wake.
16 Kisha ulichukua nguo zako na pamoja nao umepatengeneza mahali pa juu kwa ajili yako palipambwa kwa rangi tofauti tofauti, na hapo ulifanya kama kahaba. Hii haitatokea. Wala haitatokea.
17 Umevichukua vito vizuri vya dhahabu na fedha nilizowapatia, na umejitengenezea sanamu za wanaume, na umefanya pamoja nao ukahaba afanyao.
18 Ulichukua nguo zako za tarizi na kuwafunika, na kuwawekea mafuta yangu na manukato mbele yao.
19 Mkate wangu niliokupatia-ulitengenezwa kwa unga mzuri, mafuta, na asali-umeviweka mbele yao kwa ajili ya kunukia harufu nzuri, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyotokea-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
20 Kisha uliwachukua watoto wako ulionizalia, na kuwatoa sadaka kwa picha ili waliwe kama chakula. Je! matendo yako ya kikahaba ni kitu kidogo?
21 Umewachinja watoto wangu na kuwatupia kwenye moto.
22 Katika machukizo yako yote na matendo yako ya kikahaba hukutafakari kuhusu siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi na bila nguo kama kama umepigwa katika damu.
23 Ole! Ole wako! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwahiyo, zaidi ya hapo kwa haya maovu yote,
24 umejijengea chumba cha chini kwa chini katika kila sehemu ya watu wengi.
25 Umepajenga mahali pako palipoinuka kwenye kichwa cha kila njia na kuunajisi uzuri wako, kwa kuwa umeutoa mwili wako kwa kila mtu apitaye karibu na umefanya matendo mengi zaidi ya ukahaba.
26 Umetenda kama kahaba pamoja na Wamisri, tamaa ya jirani zako, na umetenda matendo mengi zaidi ya kikahaba, ili kuchochea hasira yangu.
27 Tazama! Nitakunyooshea mkono wangu na kupunguza chakula chako. Nitauchukua uhai wako juu ya adui zako, binti za Wafilisti, ambao walikuwa na haya ya tabia yako ya uchafu.
28 Umetenda kama kahaba pamoja na Waashuru kwa sababu hukuweza kuridhika. Umetenda kama kahaba na bado hukuridhika.
29 Umefanya matendo mengi zaidi ya kikahaba katika nchi ya jamii ya wana maji wa Ukaldayo, na wala hukuridhika kwa hayo.
30 Jinsi moyo wako ulivyo dhaifu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwamba utaweza kuyafanya haya mambo yote, matendo ya aibu ya kikahaba?
31 Mmepajenga mahali penu pa juu kwenye kichwa cha kila mtaa na kufanya chumba cha chini kwa chini katika kila sehemu ya watu wengi. Bado hukuwa kama kahaba kwa sababu ulikataa kulipwa ujira.
32 Wewe mwanamke mzinifu, wewe upokeaye wageni badala ya mume wako.
33 Watu hulipa kwa kila kahaba, lakini wewe huwapa mshara wako wapenzi wako wote na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote kwa matendo yako ya kikahaba.
34 Hivyo kuna tofauti kati yako na hao wanawake wengine, kwa kuwa hakuna hata mmoja ajaye kwako kukuuliza kulala pamoja nao. Badala yake, unawalipa. Hakuna akulipaye.
35 Kwa hiyo, wewe kahaba, lisikilize neno la Yahwe.
36 Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umemwaga tamaa yako na kuonyesha sehemu zako za siri kupitia matendo yako ya ukahaba pamoja na wapenzi wako wote pamoja na sanamu zako za chukizo, na kwa sababu ya damu ya watoto wako uliyowapatia sanamu zako,
37 kwa hiyo, tazama! Nitawakusanya wapenzi wako wote uliokutana nao, wote ambao uliowapenda na wote uliowachukia, na nitawakusanya juu yako kila upande. Nitawaonyesha wazi sehemu zako za siri hivyo wanaweza kuona uchi wako wote.
38 Kwa kuwa nitakuadhibu kwa uasherati na kumwaga damu, na nitaleta juu yako damu ya hasira yangu na hasira kali.
39 Nitakutia kwenye mikono yao hivyo watakutupa chini kwenye chumba cha chini kwa chini na kupavunja mahali pako pa juu na watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vyote. watakuacha uchi bila nguo.
40 Kisha wataleta kundi la watu juu yako na kukupiga kwa mawe, na kukukata kwa panga zao.
41 Watachoma nyumba zako na kufanya matendo mengi ya adhabu juu yako kwenye uso wa wanawake wengi, kwa kuwa nitakusimamisha ukahaba wako, na hutawalipa tena wapenzi wako.
42 Kisha nitatuliza ghadhabu yangu juu yako; hasira yangu itakuacha, kwa kuwa nitaridhika, na sitakuwa na hasira tena.
43 Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako na kunifanya nitetemeke kwa hasira kwa sababu ya haya mambo yote, kwa hiyo, tazama! Mimi mwenyewe nitashusha kwa kichwa chako mwenyewe adhabu kwa kile ulichokifanya-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Hutaongeza ukahaba kwa matendo yako yote ya machukizo?
44 Tazama! Kila mtu azungumzaye Mithali kuhusu wewe atasema, “Kama alivyo, hivyo pia ni binti yake.”
45 Wewe ni binti wa mama yako, amchukiaye mume wake na mtoto wake, na wewe ni dada wa dada zako aliyewachukia waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako alikuwa Mwamori.
46 Dada yako mkubwa alikuwa Samaria na binti zake walikuwa wale waliokuwa wakiishi kaskazini, wakati dada yako mdogo alikuwa ni yule aliyekuwa akiishi kusini mwako, ambaye ni, Sodoma na binti zake.
47 Hukuenenda katika njia zao na kuchukua tabia zao na matendo yao, lakini katika njia zako zote ulikuwa mbaya zaidi kuliko walivyokuwa wao.
48 Kama niishivyo- hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-dada yako Sodoma na binti zake, hawajafanya uovu mwingi kama wewe ulivyofanya na binti zako walivyofanya.
49 Tazama! Hii ilikuwa dhambi ya dada yako Sodoma: Alikuwa na kiburi katika mafanikio yake, uzembe na kutojali kuhusu chochote. Hakuitia nguvu mikono ya maskini na watu wahitaji.
50 Alikuwa na kiburi na kufanya machukizo mbele yangu, hivyo niliwatoa kama nilivyoona.
51 Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi zako; badala yake, umefanya machukizo mengi kuliko walivyofanya, na umewonyesha hayo dada zako walikuwa bora kuliko wewe kwa sababu ya machukizo yako uyafanyayo!
52 Hasa wewe, umeonyesha aibu yako mwenyewe; kwa njia hii umewaonyesha dada zako walikuwa bora kuliko wewe, kwa sababu ya dhambi ulizozifanya katika hayo machukizo yako yote. Dada zako sasa wanaonekana bora kuliko wewe. Hasa wewe, umeonyesha aibu yako mwenyewe, kwa njia hii umewaonyesha kwamba dada zako walikuwa bora kuliko wewe.
53 Kwa kuwa nitarudisha masalia wao-masalia ya Sodoma na binti zake, na masalia ya Samaria na binti zake; lakini masalia yako yatakuwa miongoni mwao.
54 Kwa kufikiria haya mambo utaonyesha aibu yako; utakuwa mnyenyekevu kwa sababu ya kila kitu ulichokifanya, na kwa njia hii utakuwa faraja kwao.
55 Hivyo dada yako Sodoma na binti zake watarudishwa kwenye hali yao ya zamani, na Samaria na binti zake watarudishwa kwenye mashamba yao ya zamani. Kisha wewe na binti zako watarudishwa kwenye hali yako ya kawaida.
56 Sodoma dada yako hakutajwa hata kwa kinywa chako katika siku ulipojiinua,
57 kabla uovu wako haujafunuliwa. Lakini sasa wewe ni kitu cha dharau kwa binti za Edomu na binti wote wa Wafilisti waliomzunguka. Watu wote wanakudharau wewe.
58 Utaonyesha aibu yako na matendo yako ya machukizo! -hivi ndivyo Yahwe asemavyo!
59 Bwana Yahwe asema hivi: Nitashughulika na wewe kama unavyostahili, wewe uliyedharau kiapo chako kwa kulivunja agano.
60 Lakini mimi mwenyewe nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe katika siku za ujana wako, nitaliimarisha agano la milele pamoja na wewe.
61 Kisha utazikumbuka njia zako na kuona aibu utakapo wapokea dada zako wakubwa na dada zako wadogo. Nitakupatia wao kama binti zako, lakini kwa sababu ya agano lako.
62 Mimi nitaweka imara agano lango pamoja nawe, nawe utajua yakwamba mimi ni Yahwe.
63 Kwa sababu ya haya mambo, utakumbuka kila kitu na kuona aibu, hutafungua mdomo wako tena kuongea kwa sababu ya aibu yako, wakati nitakapokusamehe kwa yale yote uliyoyafanya-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'