29
1 Katika siku ya kumi, katika mwezi wa kumi siku ya kumi na moja ya mwezi, neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, weka uso wako juu ya Farao, mfalme wa Misri; toa unabii juu yake na juu ya Israeli yote.
3 Nena na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Farao, mfalme wa Misri. Wewe joka kubwa ambaye ujifichaye kati ya mto, husema, “Mto wangu ni wangu mwenyewe. Nimeufanya kwa ajili yangu mwenyewe.”
4 Kwa kuwa nitaweka kalabu katika taya zako, nasamaki za mto wako zitashikamana na magamba yako; nitakuinua juu kutoka kati ya mto wako karibu na samaki zote za mto walioshikamana na maganda yako.
5 Nitakutupa chini kwenye jangwa, wewe pamoja na samaki wako wote kutoka kwenye mto wako. Utaanguka kwenye shamba la wazi; hutakusanya wala kuinua. Nitakupatia kama chakula kwa viumbe hai vya dunia na kwenye ndege wa angani.
6 Kisha wote wakaao Misri watajua kwamba mimi Yahwe, kwa sababu wamekuwa mwanzi wa kutegemewa hata kwenye nyumba ya Israeli.
7 Wakati watakapokushika kwa mkono wao, ulivunjika na kurarua wazi mabega yao; na watakapojifunza juu yako, ulivunjika, na kusababisha miguu yao kutokuwa imara.
8 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! nitaleta upanga juu yako. Nitawakatilia mbali wote mwanadamu na mnyama mbali nawe.
9 Hivyo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa. Ndipo watakapojua kwamba mimi ni Yahwe, kwa sababu jitu la kutisha liliseama, “Huu mto ni wangu, kwa kuwa nimeufanya mimi.”
10 Kwa hiyo, tazama! Ni juu yako na juu ya mto wako, hivyo nitaitoa nchi ya Misri juu ya ukiwa na jangwa, na utakuwa nchi yenye jangwa kutoka Migdoli hata Sewene na mipaka ya Kushi.
11 Hakutakuwa na mguu wa mtu kupitia, na hakuna mguu wa wanyama pori watakao upitia. Haitakuwa makao kwa miaka arobaini.
12 Kwa kuwa nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa kati ya nchi zilizoharibiwa, na miji yake kati ya miji isiyotumika itakuwa ukiwa kwa miaka arobaini; kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa, nitawatapanya kati ya nchi mbali mbali.
13 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Mwisho wa miaka arobaini nitaikusanya Misri kutoka kwa watu miongoni mwao wale waliokuwa wametawanyika.
14 Nitawarudisha wageni wa Misri na kuwarudisha hata mkoa wa Pathrosi, hata kwenye nchi ya asili yao. Kisha huko watakuwa ufalme wa chini.
15 Utakuwa chini ya falme, na hautajiinua tena juu ya mataifa. Nitawapunguza hivyo hawatatawala tena juu ya mataifa.
16 Wamisri hawatakuwa sababu kwa ajili ya imani kwa ajili ya nyumba ya Israeli. Badala yake, watakuwa kumbusho la uovu ambao Israeli umeufanya walipogeukia Misri kwa ajili ya msaada. Kisha watajua kwamba mimi ni Bwana Yahwe.”'
17 Kisha ikawa katika mwaka wa ishirini na saba siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
18 “Mwanadamu, Nebukadreza mfalme wa Babeli amelinda jeshi lake kufanya kazi ngumu juu ya Tiro. Kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega lilifanywa mali ghafi. Kisha yeye na jeshi lake hawakupokea malipo kutoka Tiro kwa kazi ngumu aliyokuwa ameimaliza dhidi yake.
19 Kwa hiyo Bwana Mungu asema hivi, 'Tazama! ninawapatia Nebukadreza nchi ya Misri mfalme wa Babeli, na atachukua utajiri wake, kuziteka nyara milki zake, na kuchukua yote atakayoyakuta huko; nayo yatakuwa mshahara wa jeshi lake.
20 Nimempatia nchi ya Misri kama mshahara kwa ajili ya kazi waliyonifanyia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
21 siku hiyo nitachipusha pembe kwa ajili ya nyumba ya Israeli, na nitakufanya uzungumze kati yao, ili kwamba wajue yakwamba mimi ni Yahwe.”'