3
1 Akanambia, “Mwanadamu, kile ulichokikuta, kula. Kula hili gombo, kisha nenda kaongee na nyumba ya Israeli.”
2 Basi nikafungua kinywa changu, na akanilisha hilo gombo.
3 Akanambia, “Mwana wa adamu, lisha tumbo lako na jaza tumbo lako kwa hili gombo ambalo nimekupa!” Basi nikalila, na lilikuwa tamu kama asali kwenye mdomo wangu.
4 Kisha akanambia, “Mwana wa adamu, nenda kwenye nyumba ya Israeli na ongea maneno yangu kwao.
5 Kwa kuwa hujatumwa kwa watu wenye maneno ya kushangaza au lugha ngumu, lakini kwa nyumba ya Israeli-
6 sio kwa taifa lenye nguvu ya maneno ya ajabu au lugha ngumu ambao maneno yao hutaweza kuyaelewa! Kama nikikutuma kwao, watakusikiliza.
7 Lakini nyumba ya Israeli haitakuwa tayari kukusikiliza, kwa kuwa hawako tayari kunisikiliza mimi. Hivyo nyumba yote ya Israeli ni paji gumu na moyo mgumu.
8 Kumbe nimeufanya uso wako kama kaidi kama nyuso zao na paji lako kuwa gumu kama mapaji yao.
9 Nimekufanya paji lako kama almasi, gumu kuliko jiwe la kiberiti! Usiwaogope wala kufadhaika kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba ya uasi.”
10 Kisha akanambia, “Mwana wa adamu, maneno yote niliyokutangazia-yachukue kwenye moyo wako na wasikize kwa sikio lako!
11 Kisha nenda kwa watumwa, kwa watu wako, na uzungumze nao. Waambie, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo; iwapo watasikia au hapana.”
12 Kisha Roho akaniinua juu, na nikasikia nyuma yangu sauti yenye tetemeko la aridhi: “Ubarikiwe utukufu wa Yahwe kutoka mahali pake!”
13 Ilikuwa sauti ya mabawa ya viumbe hai vilipokuwa vikigusana kila kimoja, na sauti ya magurudumu ambayo yalikuwa pamoja na hivyo viumbe, na sauti ya tetemeko kubwa arithi.
14 Roho akaniinua juu na kunichukua, Nikaenda kwa uchungu katika hasira kali rohoni mwangu, kwa kuwa mkono wa Yahwe ulikuwa na nguvu ukigandamiza juu yangu!
15 Hivyo nikaenda kwa watumwa huko Tel Abibu waliokuwa wakiishi karibu na Kebari Kanali, na niliishi miongoni mwao huko kwa mda wa miaka saba, kushinda kabisa katika mshangao.
16 Kisha ikatokea baada ya siku saba kwamba neno la Yahwe likanijia, likisema,
17 “Mwana wa adamu, nimekufanya uwe mwangalizi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, hivyo sikiliza neno kutoka kinywani mwangu, na uwapatie onyo langu.
18 Nitakaposema kwa waovu, 'Utakufa hakika' na usimuonye au kuzungumza onyo kwa waovu kuhusu matendo yao maovu hivyo anaweza kuishi-yule muovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.
19 Lakini kama ukimuonya muovo, na asiuache uovu wake au kutoka matendo yake maovu, kisha atakufa kwa dhambi yake, lakini utaokoa maisha yako mwenyewe.
20 Kama mwenye haki ataicha haki yake na kutenda yasiyohaki, na nikaweka kizuizi mbele yake, atakufa. Kwasababu hukumuonya, atakufa katika dhambi yake, na sintokumbuka matendo ya haki aliyoyafanya, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.
21 Lakini kama ukimuonya mwenye mtu mwenye haki kuacha kufanya dhambi halafu akaacha kutenda dhambi, ataishi hakika tangu alipo unywa; na utakuwa umeokoa maisha yako mwenyewe.”
22 Hivyo mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu huko, akanambia, “Inuka! nenda uwandani, na nitaongea na wewe huko!”
23 Nikainuka na kwenda uwandani, na huko utukufu wa Yahwe ulisimama, kama utukufu ambao niliokuwa nimeuona karibu na Kebari Kanali; hivyo nikaanguka kifudifudi.
24 Roho akaja kwangu na kusimama juu ya miguu yangu; akaongea na mimi, na kunambia, “Nenda na jifungie mwenyewe kwenye nyumba yako,
25 kwa sasa, mwana wa adamu, wataweka kamba juu yako na kukufunga ili usiweze kutoka nje miongoni mwao.
26 Nitaufanya ulimi wako ugandamane na paa ya mdomo wako, ili kwamba uwe kimya, na hutaweza kuwakemea, kwa kuwa ni nyumba ya waasi.
27 Lakini nitakapozungumza na wewe, nitafungua mdomo wako hivyo utawaambia, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.' Yeye asikiaye na asikie; yeye asiyesikia na asisikie, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi!”