7
1 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
2 Wewe, mwanadamu-Bwana Yahwe asema hivi kwa nchi ya Israeli.”'Mwisho! Mwisho umekuja kwenye mipaka minne ya nchi.
3 Sasa mwisho uko juu yako, kwa kuwa natuma ghadhabu yangu juu yako, nitakuhukumu kulingana na njia zako; nitaleta machukizo yako yote juu yako.
4 Kwa kuwa macho yangu hayatakuhurumia, na sitakuharibu. Badala yake, nitaleta njia zako zote juu yako, na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako, hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe.
5 Bwana Yahwe asema hivi: Msiba! Msiba wa pekee! Tazama, unakuja.
6 Mwisho unakuja hakika. Mwisho umeamsha dhidi yenu. Tazama! unakuja!
7 Kifo chako kinakuja kwako ukaaye kwenye nchi. Mda umefika; siku ya uharibifu iko karibu, na milima haitakuwa na shangwe tena.
8 Sasa baada ya mda mfupi nitamwaga dhahabu yangu juu yako na kujaza hasira yangu juu yako wakati nitakapokuhukumu kulingana na njia zako na kuleta machukizo yako yote juu yako.
9 Kwa kuwa jicho langu halitaona kwa huruma, sitakuharibu, kama ulivyofanya, nitafanya kwako; na machukizo yako yatakuwa katikati yako hivyo utajua kwamba ni mimi Yahwe, anayekuadhibu.
10 Tazama, siku! Tazama, inakuja! Kifo kimetoka! fimbo ya kuadhibia imechanua, kiburi kimechipua!
11 Udhalimu umekua kwenye fimbo ya udhaifu-hakuna kati yao, na hakuna katika ya kundi lao, hakuna katika utajiri wao, na hakuna wa muhimu wao atakaye baki!
12 Muda unakuja; siku imekaribia. Usimuache anayenunua shangwe, wala asihuzunike auzaye, kwa kuwa hasira yangu iko juu ya kikundi kizima!
13 Kwa kuwa muuzaji hatarudia kile kilichouzwa, kadiri wanapoendelea kuishi, kwa kuwa maono yako juu yako kikundi kizima. Hawatarudi, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi kwenye dhambi atakayejitia nguvu!
14 Wamepiga tarumbeta na kufanya kila kitu tayari, lakini hakuna mtu anayeenda kupigana; kwa kuwa hasira yangu iko juu ya kundi zima.
15 Upanga uko nje, na tauni na njaa viko nje kwenye jengo. Wale walioko shambani watakufa kwa upanga, wakati njaa na tauni zitakapowala wale waliopo kwenye mji.
16 Lakini watakao salia watatoroka kutoka miongoni mwao, na watakwenda kwenye milima. Kama hua wa mabondeni, wote watalia-kila mtu kwa ajili ya uovu wake.
17 Kila mkono utasita na kila goti litakuwa dhaifu kama maji, na watavaa nguo za magunia, na hofu kuu itawafunika,
18 na aibu itakuwa juu ya kila uso, na upara juu ya vichwa vyao vyote.
19 Watatupa fedha yao kwenye mitaa na dhahabu yao itakuwa kama jalala. Fedha yao na dhahabu yao haitaweza kuwaokoa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe. Maisha yao hayataokolewa, na njaa yao haitashiba, kwa sababu uovu wao umekuwa kizuizi.
20 Kwenye fahari yao walichukua kito yake nzuri za mapambo, pamoja nao wakatengeza sanamu zao za vinyago, na vitu vyao vichukizavyo. Kwa hiyo, nayabadilisha haya kuwa kitu najisi kwao.
21 Kisha nitawapatia hivyo vitu kwenye mikono ya wageni kama mateka na kwa waovu wa dunia kama mateka, na watapanajisi.
22 Kisha nitaugeuza uso wangu mbali kutoka kwao watakapo najisi mahali pangu pa siri; maharamia wataingia humo na kupanajisi.
23 Tengeneza mnyororo, kwa sababu nchi imejaa hukumu ya damu, na mji umejaa udhalimu.
24 Hivyo nitaleta waovu wengi wa mataifa, na watamilki nyumba zao, na nitaleta mwisho kwenye fahari ya uweza, kwenda mahali pao patakatifu patanajisiwa!
25 Hofu itakuja! Wataitafuta amani, lakini haitakuwepo.
26 Majanga juu ya majanga yatakuja juu yangu, na kutakuwa na tetesi juu ya tetesi. Kisha watatafuta ono moja kutoka kwa nabii, lakini sheria itawaangamiza kutoka kwa kuhani na shauri kutoka kwa wazee.
27 Mfalme ataomboleza na mwana wa mfalme atakata tamaa, wakati mikono ya watu wa nchi itatetemeka kwa hofu. Kulingana na njia zao wenyewe nitafanya hivi kwao! Nitawahukumu sawa sawa na wanavyostahili hadi watakapojua yakwamba mimi ni Yahwe.'”