6
1 Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
2 “Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
3 “ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”
4 Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
5 Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
6 Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
7 watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
8 mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru.
9 Na ninyi mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
10 Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani.
12 kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika sehemu za mbingu.
13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.
14 Hatimaye simameni imara. Fanyeni hivi baada ya kuwa mmefunga mkanda katika kweli na haki kifuani.
15 Fanyini hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.
16 Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale ya yule mwovu.
17 Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
18 pamoja na maombi na dua. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.
19 Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.
20 Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema.
21 Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.
22 Nimemtuma kwenu kwa kusudi hili maalumu, ili kwamba mjue mambo kuhusu sisi, aweze kuwafariji mioyo yenu.
23 Amani na iwe kwa ndugu, na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.
24 Neema na iwe pamoja na wote wanampenda Bwana Yesu Kristo kwa pendo lile lisilo kufa.