3
1 Ilikuwa miezi saba baaada ya watu wa Israeli kurudi kwenye miji yao, ndipo walipojikusanya pamoja kama mtu mmoja katika Yerusalem.
2 Yeshua mwana wa Yosadaki na kaka yake kuhani, na Zerubabeli mwana wa Sheatieli na kaka yake wakainuka na kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli na kutoa sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa katika sheria ya Musa, Mtu wa Mungu.
3 Ndipo wakaanzisha madhabahu juu ya msingi, kwa hofu waliokuwa nayo kwa sababu ya watu wa nchi/ Wakatoa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe asubuhi na jioni.
4 Pia vilevile wakaichunguza sikukuu ya vibanda kama ilivyoandikwa na wakatoa sadaka ya kuteketezwa siku kwa siku kama ilivyoagizwa, kila siku kwa siku yake.
5 Kulikuwa na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa na mwezi mara moja na sadaka za siku ya Yahwe za kudumu, pamoja na sadaka zote za hiari.
6 Walianza kutoa sadaka za kuteketezwa za Yahwe siku ya kwanza ya mwezi wa saba, ingawa hekalu lilikuwa halijaanza kujengwa.
7 Hivyo wakatoa fedha kwa wahunzi na fundi wa mkono, na wakawapa chakula, vinywaji na mafuta kwa watu wa Sidoni na Tiro, ili kwamba walete miti ya mierezi kupitia baharini kutoka Lebanoni mpaka Yafa, na kama walivyo ruhusiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi.
8 Ndipo mwezi wa pili katika mwaka wa pili baadae wakaja kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem, Zerubabeli, Yoshua mwana wa Yosadaki, na baadhi ya makuhani na walawi na wale walikuja kutoka uhamishoni kurudi Yerusalem wakaanza kazi. Wakawachagua walawi walikuwa na miaka ishirini na zaidi kusimamia kazi ya nyumba ya Yahwe,
9 Yoshua akamsimamisha kijana wake na kaka yake, Kadmiel na watoto wake, na kizazi cha yuda kusimamia kufanya kazi katika nyumba ya Mungu. Pamoja na wao kulikuwa na wana wa Henadadi, na uzao wao, na pia jamaa zao walawi.
10 Wajenzi wakasimamisha msingi wa Hekalu la Yahwe, Na hii ikawawezesha makuhani kusimama na mavazi yao wakiwa na tarumbeta, na walawi wana wa Asafu, kumtukuza Yahwe kwa matoazi, kama mkono wa mfalme Daudi wa Israel alivyoagiza.
11 Waliimba kwa kumsifu na kumshukuru Yahwe. “Yeye ni mwema! Agano lake ni kweli kwa Israel ladumu milele.”Watu wote wakapiga kelele kwa sauti kuu za shangwe wakimsifu Yahwe kwa sababu misingi ya Hekalu ilikuwa imekamilika.
12 Lakini wengi wa Makuhani, walawi, wakuu wa kale, na wazeee wa zamani walioiona nyumba ya kwanza, wakati misingi ilipowekwa wakaishuhudia kwa macho yao, walilia kwa sauti. Lakiniwengi walipiga kelele kwa sauti za shangwe na furaha na sauti za kushangaza.
13 Na matokeo yake, watu hawakuweza kutofautisha sauti za furaha na sauti za shangwe na sauti za watu waliokuwa wanalia, kwa kuwa watu walikuwa wanalia kwa sauti kuu ya shangwe na sauti ilisikika kutoka mbali.