8
1 Hawa ni viongozi wa watangulizi familia ambazo zilitoka babeli pamoja nami kipindi cha utawala wa mfalme Artashasta.
2 Mwana wa Finehasi, Gershoni. Mwana wa Ithamari, Daniel. Mwana wa Daudi, Hatushi ambaye ni mwana Shekania,
3 ambaye pia ni mwana wa Paroshi na Zekaria na pamoja na yeye kulikuwa na wanaume mia moja na hamsini walitajwa kwenye idadi ya ukoo wake.
4 Wana wa Pahath- Moabu, Eliehoenai mwana wa Zerahia na pamoja naye wanaume mia mbili. Wana wa
5 Shekaniah, Yahazieli na pamoja naye wanaume mia tatu. Wana wa
6 adini, Ebedi mwana wa Yonathani na pamoja naye waliorodheshwa wanaume hamsini.
7 Wana wa Elamu, Yeshaya mwana wa Athalia na pamoja naye waliorodheshwa wanaume sabini.
8 Wana wa Shefatia, Zebadia, mwana wa Mikaeli na pamoja naye waliorodheshwa wanaume themanini.
9 Wana wa Yoabu, Obadia mwana wa Yehieli pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia mbili kumi na wanane. Wana wa Binui,
10 Sheromithi, mwana wa Yosifia na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na sitini.
11 Wana wa Bebai, zekaria mwana wa Bebai na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume ishirini na wanane.
12 Wana wa Azgadi, Yohana mwana wa Hakatani na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na kumi.
13 Wale wana wa Adonikamu wakaja baadaye. Na haya ndio majina yao: Elifereti, Yeueli na Shemaya na pamoja na wao wakaja wanaume sitini.
14 Wana wa Bigwai, Uthai, mwana wa zabudi na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume sabini
15 Nikawakusanya wasafiri bandari iliyokuwa inaelekea Ahava. Tukaweka kambi muda wa siku tatu, nikawachunguza watu na makuhani, lakini sikuwaona wana wa Levi miongoni.
16 Hivyo nikatuma kwa Eliezeri, arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu na Elnathani na Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na kwa Yoyaribu na Elnathani ambao walikuwa ni walimu.
17 Tena nikawatuma kwa Ido, kiongozi wa Kasifia. Nikawaaambia kile watachomweleza Ido. na jamaa zake, watumishi wa Hekalu waliishi Kasifia, kwa hiyo, kutuma kwetu watumishi kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
18 Hivyo wakatutuma sisi kwa Mungu na mkono mzuri wa mtu aliyeitwa Ishekeli. Alikuwa mwana wa mali Mwana wa Levi mwana wa Israel. Akaja na wana kumi na wanane na ndugu,
19 pamoja naye Hashabia, pamoja na Yeshaya wa wana wa Merari na ndugu zake na wana wake jumla watu ishirini wote. Miongoni
20 mwao walichaguliwa kutumika katika Hekalu, ambapo Daudi na wakuu waliwapa kuwahudumia walawi: mia mbili ishirini kila mmoja wao aliagizwa kwa majina.
21 Tena nikatangaza kufunga mto Ahava ili kujinyenyekeza mbele za Mungu, kutafuta njia iliyoonyoka kutoka kwake kwa ajili yetu, watoto wetu na mali zetu,
22 Niliona aibu kumwomba mfalme kwa ajili ya jeshi au mpandafarasi kwa ajili ya kutulinda tunapokuwa njiani, tangu tumemwambia mfalme “mkono wa Mungu uko pamoja na wote wanaomtafuta kwa mazuri. lakini uweza wake na ghazabu yake ni juu ya wale wote wanaomwasi yeye.
23 Hivyo tulifunga na kumsihi Mungu kwa jambo hilo.
24 Tena nikachagua watu kumi na wawili kutoka kwa kuhani: Sherebia na Hashabia na ndugu zao wengine kumi.
25 Nikapima kwa ajili yao fedha, dhahabu na vyombo na sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu kwa wafalme, washauri, na wakuu na Israel wote walitoa kwa hiari.
26 Hivyo nikawapimia kwenye mikono yao talanta za fedha mia sita na hamsini, talanta mia moja ya vyombo vya fedha, talanta mia moja za dhahabu.
27 vifaa ishirini vya dhahabu kwa pamoja vilikuwa na thamani ya elfu moja darkoni na vitu viwili vya sanamu vivyonakshiwa kama dhahabu ya kupendeza.
28 Kisha nikawaambia, mmewekwa wakfu kwa Bwana, na hivi vyombo pia na fedha na dhahabu, vimetolewa kwa hiari kwa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu.
29 mviangalie na kuvitunza hadi mtakapovipima mbele ya makuhani, walawi, na viongozi wa wataangulizi wa jamii ya Israel katika Yerusalem katika nyumba ya Mungu.
30 Makuhani na walawi walikubali vipimo vya fedha na dhahabu na vyombo kwa ajili ya kuvichukua na kuvipeleka Yerusalem, kwenye nyumba ya Mungu wetu.
31 Tukatoka kwenda mto Ahava siku ya kumi na mbili katika mwezi wa kwanza kwenda Yerusalem, Mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, ulitulinda na mikono ya adui na wale waliotaka kutufanyia fujo njiani.
32 Hivyo tukaingia Yerusalem na kukaa humo kwa siku tatu.
33 Tena siku ya nne fedha na dhahabu na vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa mikono ya Meremothi mwana wa Uria kuhani, na pamoja nao alikuwepo Eleazari mwana wa Finehasi, Yozabadi mwana wa Yeshua, na Noadia mwana wa Binui, Walawi.
34 Idadi na uzito wa kila kitu uliweza kujulikana. Uzito wote uliweza kuandikwa katika kipindi hicho
35 Na wale waliokuja kutoka matekani, watu wa uhamisho, wakatoa sadaka ya kutekezwa kwa Mungu wa Israel, kondoo tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi wa kiume kumi na wawili kama sadaka ya dhambi. Zote zilikuwa sadaka za kutekezwa kwa ajili ya Yahwe.
36 Tena wakawapa amri za mfalme kwa wakuu wa wafalme na wakuu katika mji ngambo ya mto, na wakawasaidia watu na nyumba ya Mungu.