36
1 Hivyo Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Yahweh aliye mpa ustadi na uwezo kujua jinsi ya kufanya kazi katika ujenzi wa sehemu takatifu wafanye kazi kadiri ya yote Yahweh aliyo amuru.”
2 Musa akamuita Bezaleli, Oholiabu, na kila mtu mwenye ujuzi ambaye Yahweh kampa ujuzi, na ambaye moyoni mwake ulichochewa kuja na kufanya kazi.
3 Walipokea kutoka kwa Musa sadaka zote ambazo Waisraeli walizo leta kwa ujenzi ya sehemu takatifu. Watu walikuwa bado wanaleta sadaka za hiari kila asubui kwa Musa.
4 Hivyo watu wote walikuwa na ujuzi walikuwa wakifanya kazi sehemu takatifu walikuja kutoka kwenye kazi walikuwa wakifanya.
5 Wachonga mawe walimwabia Musa, “Watu wanaleta zaidi sana ya yanayo itajika kufanya kazi Yahweh aliyo tuamuru.”
6 Hivyo Musa akaamuru mtu yeyote asilete tena kwa ujenzi wa sehemu takatifu. Kisha watu wakaacha kuleta hivi vitu.
7 Walikuwa na zaidi ya vitu vya ujenzi.
8 Hivyo wachonga mawe miongoni mwao wakajenga lile hema la kuabudia kwa mapazia kumi yaliyo jengwa kitamba kizuri na buluu, zambarau, na sufu nyekundu kwa aina ya kerubi. Hii ni kazi ya Bezaleli, mjenzi mwenye ujuzi sana.
9 Urefu wa kila pazia ulikuwa mikono ishirini na nane, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa vyote hivyo vilikuwa na kipimo kimoja.
10 Bezaleli akaunganisha vitambaa vitano pamoja, na vile vitambaa vingine vitano akaviunganisha pamoja.
11 Kisha akafanya vitanzi vya uzi wa bluu kwenye upindo wa kitambaa kilicho mahali pa kuungania. Akafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pale pengine pa kuungania.
12 Akafanya vitanzi hamsini kwenye kitambaa kimoja, akafanya vitanzi hamsini kwenye mwisho wa kitambaa kilichokuwa mahali pale pengine pa kuungania, vitanzi hivyo vikiwa vinaelekeana.
13 Mwishowe akafanya kulabu hamsini za dhahabu na kuviunganisha vitambaa hivyo pamoja kwa kulabu hizo, hivi kwamba hiyo ikawa maskani moja.
14 Bezaleli akafanya vitambaa vya mahema vya manyoya ya mbuzi kwa ajili ya hema lililo juu ya maskani. Vitambaa kumi na moja ndivyo alivyofanyiza.
15 Urefu wa kila kitambaa ulikuwa mikono thelathini, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa hivyo kumi na moja vilikuwa na kipimo kimoja.
16 Kisha akaunganisha vitambaa vitano pamoja na vile vitambaa vingine sita pamoja.
17 Kisha akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pa kuungania, naye akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kile kitambaa kingine kilichoungana nacho.
18 Bezaleli akafanya kulabu hamsini za shaba kwa ajili ya kuliunganisha hilo hema pamoja liwe kipande kimoja.
19 Naye akafanya kifuniko cha hema kutokana na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko kutokana na ngozi za sili, upande wa juu.
20 Bezaleli akafanya viunzi vya mbao vya hema ya kukutani kutokana na mbao za mshita.
21 Urefu wa kiunzi ulikuwa mikono kumi, nao upana wa kila kiunzi ulikuwa mkono mmoja na nusu.
22 Kila kiunzi kilikuwa na ndimi mbili zilizounganishwa. Hivyo ndivyo alivyofanya viunzi vyote vya maskani.
23 Basi akafanya viunzi vya maskani, viunzi ishirini kwa ajili ya upande kuelekea kusini.
24 Bezaleli akafanya vikalio arobaini vya fedha viwe chini ya vile viunzi ishirini, vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja pamoja na ndimi zake mbili na vikalio vingine viwili chini ya kiunzi kingine pamoja na ndimi zake mbili.
25 Na kwa ajili ya ule upande mwingine wa maskani, upande wa kaskazini, akafanya viunzi ishirini
26 na vikalio vyake arobaini vya fedha. Vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio viwili chini ya kiunzi kingine
27 Na kwa ajili ya zile pande za nyuma za maskani kuelekea magharibi akafanya viunzi sita.
28 Naye akafanya viunzi viwili vya pembeni ya maskani kwenye pande zake mbili za nyuma
29 Hizi zilikuwa pacha upande wa chini, lakini juu ya kila moja kwenye pete ya kwanza. Hivyo ndivyo alivyoifanya yote miwili, ile miimo ya pembeni.
30 Basi vikajumlika kuwa viunzi vinane na vikalio vyake kumi na sita vya fedha, vikalio viwili kando ya vikalio viwili chini ya kila kiunzi.
31 Bezaleli akafanya miti ya mshita, mitano kwa ajili ya viunzi vya upande mmoja wa maskani,
32 na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya upande ule mwingine wa maskani na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya maskani kwa ajili ya zile pande mbili za nyuma za magharibi.
33 Kisha akafanya mti wa katikati upitie katikati ya vile viunzi toka mwisho mmoja mpaka ule mwingine.
34 Naye akavifunika vile viunzi kwa dhahabu, akafanyiza pete zake za dhahabu ziwe vitegemezo kwa ajili ya ile miti, akaifunika ile miti kwa dhahabu.
35 Bezaleli akafanya pazia, la uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa cha rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kalitia makerubi kwa kazi ya mjenzi.
36 Kisha akalifanyia nguzo nne za mshita na kuzifunika kwa dhahabu, vibanio vyake vikiwa vya dhahabu, na kutengeneza vikalio vinne vya fedha kwa ajili yake.
37 Naye akafanya kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema kutokana na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kazi ya mfumaji.
38 Pia akafanya na nguzo zake tano na vibanio vyake. Naye akavifunika vilele vyake na viungo vyake kwa dhahabu, lakini vile vikalio vyake vitano vilikuwa vya shaba.