10
1 Israeli ni mzabibu mzuri ambao huzaa matunda yake. kwa kadiri matunda yake yanavyoongezeka vivyo hivyo anajenga madhabahu nyingi. Kwa kuwa nchi yake ilizalishwa zaidi, aliboresha nguzo zake.
2 Moyo wao ni udanganyifu; sasa wanapaswa kubeba hatia yao. Bwana ataharibu madhabahu zao; ataharibu nguzo zao.
3 Kwa maana watasema, “Hatuna mfalme, kwa maana hatukumcha Bwana. Na mfalme-angeweza kutufanyia nini?”
4 Wanasema maneno tupu na kufanya maagano kwa kuapa uongo. Kwa hivyo haki inakuja kama magugu yenye sumu katika mito ya shamba.
5 Wakazi wa Samaria wataogopa kwa sababu ya ndama za Beth Aveni. Watu wake waliomboleza juu yao, kama walivyofanya wale makuhani wa sanamu ambao walikuwa wamefurahi juu yao na utukufu wao, lakini hawako tena.
6 Wao watachukuliwa kwenda Ashuru kama sadaka kwa mfalme mkuu. Efraimu atakuwa na aibu, na Israeli atakuwa na aibu kwa sanamu yake.
7 Mfalme wa Samaria ataangamizwa, kama chipu cha kuni juu ya uso wa maji.
8 Sehemu za juu za uovu zitaharibiwa. Hii ndiyo dhambi ya Israeli! Miti na vichaka vitakua juu ya madhabahu zao. Watu wataiambia milima, “Tufunike sisi!” na kwa vilima, “Tuangukieni!”
9 Ee Israeli, umetenda dhambi tangu siku za Gibea; huko umebaki. Je, vita vitawapata wana wa uovu huko Gibea?
10 Nitakapotaka, nitawaadhibu. Mataifa wataungana pamoja nao na kuwaweka katika vifungo kwa uovu wao mara mbili.
11 Efraimu ni ndama mwenye mafunzo ambayo anapenda kupura nafaka, hivyo nitaweka jozi juu ya shingo yake nzuri. Efraimu nitauweka jozi; Yuda ataimea; Yakobo atauvuta pigo kwa nafsi yake.
12 Jifanyieni haki, vuneni matunda ya uaminifu wa agano. Chimbueni ardhi yenu isiyopandwa, kwa maana ni wakati wa kumtafuta Bwana, mpaka atakapokuja na kuinua haki juu yenu.
13 Mmelima uovu; mmevuna udhalimu. Mmekula matunda ya udanganyifu kwa sababu uliamini katika mipango yako na katika askari wako wengi.
14 Kwa hiyo mlipuko wa vita utafufuka kati ya watu wako, na miji yako yote yenye ngome itaharibiwa. Itakuwa kama Shalmani aliharibu Beth Arbeli siku ya vita, wakati mama alivunjika vipande vipande na watoto wake.
15 Kwa hiyo itakuwa kwako, Betheli, kwa sababu ya uovu wako mkubwa. Wakati wa mchana mfalme wa Israeli atakatwa kabisa.