3
1 Bwana akaniambia, “Nenda tena, mpendeni mwanamke, aliyependwa na mumewe; lakini ni mzinzi. Mpende kama mimi, Bwana, ninavyowapenda watu wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine na kupenda mikate ya zabibu.”
2 Kwa hiyo nimemnunulia mwenyewe kwa vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri.
3 Nilimwambia, “Lazima uishi pamoja nami siku nyingi. Huwezi kuwa kahaba au kuwa na mtu mwingine yeyote. Kwa njia hiyo hiyo, nitakuwa pamoja nanyi.”
4 Kwa maana wana wa Israeli wataishi kwa siku nyingi bila mfalme, mtu mkuu, dhabihu, nguzo ya mawe, efodi au sanamu za nyumbani.
5 Baadaye watu wa Israeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Na katika siku za mwisho, watakuja wakitetemeka mbele za Bwana na wema wake.