12
1 Siku hiyo utasema, ''Nitakushukuru wewe, Yahwe. Japo ulikuwa na hasira na mimi, laana yako imeondoka mbali, na umenifariji mimi,
2 Ona Bwana ni wokovu wangu; nitamwamini na sitakuwa na hofu, kwa Yahwe, ndio, Yahwe ni nguvu yangu na wimbo wangu. Amekuwa wokovu wangu.''
3 Kwa furaha utachota maji kwenye kisima cha wokovu.
4 Siku hiyo utasema, ''Mshukuru Yahwe na ita jina lake; tangaza matendo yake miongoni mwa watu, tangaza jina lake limeinuliwa.
5 Mwiimbie Yahwe, maana ametenda matendo yaliotukuka; acha hili lijulikane dunia nzima.
6 Lia kwa nguvu na piga kelele kwa furaha, enyi wakazi wa Sayuni, maana katikati yenu ni mtakatifu wa Israeli.