19
1 Tamko kuhusu Misri. Ona, Yahwe atasafiri katika mawimbi mepesi na anakuja Misri; Sanamu za Misri zitatemeka mbele yake, na mioyo ya Wamisri itayeyuka ndani yao wenyewe.
2 Nitawachanganya Wamisri juu dhidi ya Wamisiri: Mtu atapigana dhidi ya ndugu yake, mji dhidi ya miji, na ufalme dhidi ya ufalme.
3 Roho ya Misri itadhohofishwa kutoka ndani. Nitauharibu ushauri wake, japo wanafikiria ushauri wa sanamu, roho za watu waliokufa, na mizimu, na
4 Nitawacha Wamisiri kwenye mikono ya viongozi wakatili, kiongozi imara atawaongoza wao- Hili ni tamko la Yahwe Bwana wa majehi.''
5 Maji ya bahari yatakauka juu, na mto uakauka na kuwa mtupu.
6 Mito itakuwa michafu; mikondo ya Misri itakuwa dhii na kukauka; mwanzi na bendera zake zitapeperushwa mbali.
7 Mianzi ya Nile, kwa mdomo wa mto Nile, na mbegu zote zitakazo katika mashamba ya Nilezitakauka zote, zitageuka kuwa mavumbi, na kupeperukia mbali.
8 Wavuvi watalia na kuomboleza, na wale watakao shusha neti kwenye maji watauzunika.
9 Wafanyakazi ya kuchana kitani watafaidika na hao washonao nguo nyeupe watajeuka kuwa mchonaji.
10 Washona nguo wa Misri wataangamizwa; na wote waloajiriwa watahuzunika nafsini mwao.
11 Wakuu wa Zoana ni wajinga kabisa. Washauri wenye busara wa Farao ni wapumbavu. Unawezaje kumwambia Farao, ''Mimi ni mtoto wa watu wenye busara,
12 ''Wako wapi hao watu wenye busara? mtoto wa mfalme wa zamani? Waache wakuambie? na ijulikane kitu ambacho Yahwe wa majeshi amekipanga kuhusiana na Misri.
13 Wakuu wa Zoani wamekuwa wajinga, wakuu wa Memphisi wamegawanyika; wameifanya Misri iende kinyume, na mawe ya pembeni ya makabila yao.
14 Yahwe amechanganya roho wa kuvurugwa katika yao, na wamefanya Wamisri kwenda kinyume kwa yote wanoyafanya, kama mlevi anavyoyumbayumba uku akitapika.
15 Hakuna kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukifanya kwa ajili ya Misri, kama kichwa au mkia, tawi au mwanzi.
16 Siku hiyo, Wamisri watakuwa kama wanawake. watatemeka na kuogopa mkono wa Yahwe wa majeshi ulioinuliwa juu yao.
17 Nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri. Yeyote atakao wakumbusha wao kuhusu yeye, wataogopa sana, kwa sababu ya mpango wa Yahwe, anaoukusudia juu yao.
18 Siku hiyo kutakuwa na miji mitano katika nchi ya Misri wanaozungumza lugha ya Kanaani na kuapa kimtii Yahwe wa majeshi. Moja kati ya miji hii itaitwa mji wa ulioharibiwa.
19 Siku hiyo kutakuwa madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika ya nchi ya Misri, na jiwe la chumvi karibu na Yahwe.
20 Itakuwa kama ishara na ushahidi kwa Yahwe wa majeshi katika nchi ya Misri. Atawatumia mkombozi na mlinzi, na atawokoa wao.
21 Yahwe atajulikana Misri, na Wamisri watamkubali Yahwe siku hiyo. Watamuabudu kwa sadaka na matoleo, na wataweka agano na kulitimiza.
22 Yahwe ataipga Misri, ataipiga na kuiponya. Halafu watamrudia Yahwe; atasikiliza maombi yao na kuwaponya.
23 Siku hiyo kutakuwa na njia kuu kutoka Misri kwenda Asiria, na Waasira watakuja Misri, na Wamisri watakwenda Asira; na Wamisri wataabudu pamoja na Waasiria.
24 Siku hiyo, Israeli itakuwa ya tatu pamoja na Misri na Asiria, baraka katikati ya nchi;
25 Yahwe wa majeshi atawabariki na kusema, '' wabarikiwe Wamisri, watu wangu; Wasiria, kazi ya mikono yangu; na Israeli urithi wangu.