25
1 Yahwe wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe, nitalisifu jina lako; maana umetenda matendo ya ajabu, mambo uliyoyapanga toka zamaini, kwa uaminifu na ukamilifu.
2 Maana umeufanya mji kuwa chungu, ngome ya mji, uharibifu na ngome ya wageni kuwa si mji.
3 Hivyo basi watu wenye nguvu watakutukuza wewe; na mji waishio watu wasio na ukatili watakuogopa wewe.
4 Maana umekuwa katika eneo salama kwa aliye masikni, makazi kwa mhitaji ambaye yuko kwenye dhiki- makazi kwa aliyeko kwenye dhoruba na kivuli kwa aliyeko kwenye jua. Pale punzi ya watu wakatili imekuwa kama dhoruba dhidi ya ukuta,
5 na jua kwenye aridhi kavu, na watazuia kelele za wageni, kama vile jua linavyozuiliwa na kivuli cha mawingu, hivyo basi nyimbo wasio na makosa zimejibiwa.
6 Katika mlima huu Yahwe wa majeshi atafanya kwa watu sikukuu ya ya vitu vilivyonona, na mvinyo uliochaguliwa, zabuni ya nyama na sikuku juu ya sira.
7 Na katika mlima huu atauharibu mfuniko uliowekwa juu watu wote, na mtandao wa kusuka juu ya mataifa.
8 Atameza kifo daima, na Bwana Yahwe atayafuta machozi katika nyuso zetu; na aibu ya watu wake itatupwa mbali kutoka duniani kote, maana Yahwe amesema hivyo.
9 Yatazungumzwa katika siku hiyo, ''Huyu ni Mungu wetu; na tunayemngoja, na atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tuliyemngoja, tutafurahia na kushangilia wokovu wake.''
10 Maana katika mlima huu mkono wa Bwana utashuka; na Moabu itakanyagwakangwa chini kwenye eneo lake, na hata majani yatakanyagwakanyagwa chini katika shimo lililojaa mbolea.
11 Wataitawnya mikono yao katikati yao, kama vile mpiga mbizi atawanyavyo mikono yake wakati akipiga mbizi. Lakini Bwana atashusha kiburi chao chini japo kuwa na ujuzi katika mikono yao.
12 Na ataiangusha chini kwenye aridhi kuta za ngome, kwenye mavumbi.