38
1 Siku zile Hezekia alikuwa anaumwa karibia na kufa. Hivyo Isaya mtoto wa Amozi, nabii alikuja kwake na kumwambia, ''Yahwe amesema, 'panga mambo yako maana utakufa, hautaishi.'
2 'Halafu Hezekia akaugeukia ukuta na akamuomba Yahwe.
3 Na akasema, ''samahani Yahwe, kumbuka jinsi nilivyoenenda kwa uaminifu mbele zako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya matendo mema katika macho yako.'' Na Hezekia akalia kwa sauti.
4 Basi neno la Yawe likamjia Isaya, na kusema,
5 ''Nenda ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ''Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yenu, amesema: Nimeyasikiliza maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Ona ninakaribia kuongeza miaka kumi na tano katika maisha yako.
6 Na nitakukomboa wewe pamoja mji huu kutoka kwenye mkono wamfalme wa Asiria, na nitaulinda huu mji.
7 Na hii itakuwa alama kwako kutoka kwangu, Yahwe, kwamba nitafanya nilichokisema:
8 Angalia, nitasababisha kimvuli katika nyumba ya Ahazi kwenda nyuma hautua kumi.'' hivvyo basi kivuli kilirudi nyuma hatua kumi juu ya nyumba iliyopanda juu.
9 Haya ndiyo maandishi ya maombi ya Hezekia mfalme wa Yuda, alipokuwa anaumwa halafu akapona:
10 ''Nimesema kwamba nusu ya maisha yangu nitapita katika mlango wa kuzimu; Nilitumwa pale miaka yangu yote.
11 Nikasema sitamuona tena Yahwe, Yahwe kaika nchi ninayoishi; sitaangalia watu tena au wenyeji wa dunia hii.
12 Maisha yangu yameondolea na kupelekwa mbali na mimi kama hema la mchungaji; Niliyakunja maisha yangu juu kama mfumaji; ameniondoa katika kifungo; kati ya mchana na usiku ameyakomesha maisha yangu.
13 Nililia mpaka asubuhi; kama simba anaivunja mifupa yangu. Kati ya usiku na mchana ameyakomesha maisha yangu.
14 Kama mbayuwayu ndivyo nilivyolia; nililia kama njiwa; macho yangu yalichoka kuangalia juu. Bwana ninateseka; nisaidie mimi.
15 Niseme nini? wote wameongea na mimi na amefanya hivyo; Nitatembea taratibu miaka yangu yote maana ninayashinda kwa huzuni.
16 Bwana, mateso uliyoyatuma ni mazuri kwangu; ikiwezekana nirudishiwe tena maisha yangu; umeyahifadhi maisha maisha yangu na afya yangu.
17 Ni kwa faida yangu kwamba nimwpitia huzuni kama hii. Umenikomboa kutoka kwenye shimo la uharibifu; maana umetupa dhambi zangu nyuma yako.
18 Maana kuzimu hapata kushukuru wewe; kifo hakikusifu wewe; wale wote waendao ndani ya shimo hawana matumaini ya uaminifu wako.
19 Mtu anayeishi, mtu anayeishi, ndiye anayekushukuru wewe, kama ninavyofanya leo; baba atawjulisha watoto uaminifu wako.
20 Yahwe anakarbia kunikomboa mimi, na tutasherekea kwa mziki siku zote za maisha yetu katika nyumba ya Yahwe.''
21 Sasa Isaya alisema, ''Waacheni wachukue donge mitini na kuliweka kweye jipu naye atapona.
22 ''Hezekia pia alisema, ''Je ni ishara gan ya kwamba nitaiende juu katika nyumba ya Yahwe?''