41
''Sikilizeni mbele yangu kwa ukimya, enyi mkao pwani; wacha mataifa yapate nguvu kwa upya; waache waje karibu na kuzungumza; na tusogee karibu tujadili mgogoro. Nani aliyechochea juu mmoja kutoka mashariki, anamuita katika haki yake kwenye huduma yake? Amemkabidhi mataifa juu yake ili amsaidie yeye kuwaangamiza wafalme. Aliwajeuza kuwa mavumbi kwa neno lake, kama upepo unaovuma kwenye mabua kwa upinde wake. Aliwachukuwa wao na kuwapitisha salama, katika njia nyepesi ambayo miguu yake imegusa shida. Ni nani aliyeyafanya na kukamilisha matendo haya? Ni nanialiyechagua kizazi kutoka mwanzo? Mimi, Yahwe ni mwanzo na mwisho, mimi ndiye. Visiwa vimeona na kuogopa; miisho ya dunia yatetemeka; walikaribia n kuja. Kila mmoja amsaidie jirani yake, na kila mmoja asemezane na mwenzake, 'Kuwa mfariji; Hivyo basi seremala anamfariji mfua dhahabu, na yule anayefanya kazi kwa kutumia nyundo anamfariji anayefanya kazi kwa chuma, akisema kwa msemo wa kurehemu, ''Ni mizuri; Naye ataupigilia kwa makini misumari ili isipinduke. Lakini wewe, Israeli mtumishi wangu, Yakobo niliyekuchagua, mtoto wa Ibrahimu rafiki yangu, wewe ambaye ninakurudisha kutoka miisho ya nchi, na ambaye niliyekuita kutoka sehemu ya mbali, na kwako niliyekuambia, 'Wewe ni mtumishi wangu,; 'Nimekuchagua wewe na sijakukataa. 10 Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu. 11 Tazama, watakuwa na aibu na hawataheshimiwa, wale wote waliokuwa na hasira na wewe; watakuwa si kitu na watatokomea, wale watakao kupinga wewe. 12 Utawatafuta na wala hautawapata wale wanaopingana na wewe; wale wafanyao vita dhidi yako watakuwa kama si kitu, si kitu kabisa. 13 Maana mimi Yahwe Mungu wako, nitawashika mkono wako wa kiume, nikikuambia wewe, 'Usiogope; Nitakusaidia wewe. 14 Usiogope, Yakobo wewe mdudu, na enyi watu wa Israeli; Nitawasaidia''- hili ni tamko la Yahwe, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli. 15 Tazama, ninakufanya wewe kuwa chombo kikali cha kuparulia chenye makali pande mbili; utaparua milima na kuiponda; utafanya vilima kama makapi. 16 Utawatawanya wao, na upepo utawabeba na kuwapeka mbali; upepo utawatanya wao. Utashanglia katika Yahwe, utashangiliakatika mtakatifu wa Israeli 17 Waliodhulumiwa na masikini wanatafuta maji, lakini hakuna kitu, ndimi zao zimekauka kwa kiu; Mimi Yahwe, nitajibu maombi yao; Mimi Mungu wa Israeli, sitawacha wao. 18 Nitatengeneza mikondo ya maji kushusha chini, na chemichem katikati ya mabonde; nitalifanya jangwa kuwa kisima cha maji, na aridhi kavu kuwa chemichem ya maji. 19 Katika jangwa nitapanda mierezi, mshita, mhadisi, na mti wa mizeituni. Nitaotesha mberoshi katika uwazi wa jangwa, pamoja na mbono nitapanda mberoshi kitika jangwa lililowazi. 20 Nitayafanya haya ili waweze kuona, kutambua na kuelewa kwa pamoja, kwamba mkono wa Yahwe umetenda haya, kama Mtakatifu wa Israeli aliyeliumba. 21 Wakilisha keshi yako, '' asema Yahwe; ''wakilisha hoja zenu nzuri kwa sanamu yenu,'' asema Mfalme wa Yakobo. 22 Waache walete hoja zao wenyewe; waache waje mbele na watutangazie sisi nini kitakachotokea, ili tuweze kuelewa haya mambo vizuri. Tuawaache watupe tamko mapema, ili tuweze kulitafakari na tuweze kujua n kwa jinsi gani litatimia. 23 Wajulishe kitu kuhusu baadaye, ili tujue kuwa ninyi ni miungu; fanya kitu kizuri au kibaya, ambacho kitatutisha na kutushangaza. 24 Tazama sanamu zenu si kitu na matendo yenu si kitu; aliyewachagua ni machukizo. 25 Nimemnyanyua mmoja kutoka kaskazini, naye amekuja kutoka mawio ya jua nimemchagua yeye alitajae jina langu, na atawakanyaga viongozi kama matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo. 26 Ni nani aliyetangaza hili tangu mwanzo, ili tuweze kujua? na kabla ya mda, ili tuseme, ''Yuko sawasawa''? Kweli hakuna hata mmoja aliyekiri hili, ndio hakuna hata mmoja aliyekusikia ukisema chochote. 27 Kwanza nilizungumza na Sayuni, ''Tazama hapo walipo;'' Nimemtuma mhubiri Yerusalemu. 28 Nilipoangalia, hakuna hata mmoja, hakuna hata miongoni mwao ambaye anaweza kutoa ushauri mzuri, nani, lini nimulize, awezaye kunijibu neno. 29 Tazama, matendo yao si kitu; sanamu zao za chuma zilizotupwa ni upepo na utupu.