46
1 Beli huaguka chini, Nebo husujudu; miungu yao imebebwa na wanyama na mzigo wa mnyama. Sanamu hizi mlizobeba ni mzigo mzito kwa wanyama kuchoka.
2 Kwa pamoja wanashuka chini; hawawezi kuziokoa sanamu zao, na wao wenyewe wameenda uhamishoni.
3 Nisikilizeni mimi, nyumba ya Yakobo, wote mliobaki kwenye nyumba ya Israeli mliochukuliwa na mimi kutoka kabla amjazaliwa, mlichukuliwa mkiwa tumboni.
4 Hata kwa njie wazee Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitwachukua nyie na nitawakomboa nyie.
5 Je utanifananisha mimi na nani? na mimi nimefanana na nani, ili utulinganishe?
6 Watu humwaga dhahabu kutoka kwenye mabegi yao na uzito wa fedha kwenye uzani. Humuajiri mfua dhahabu, na hutengeneza kuwa dhahabu; na huinama chini na kuzisuju.
7 Wanazinyanyua juu ya mabega yao na kuzibeba; wanaziweka katika sehemu yake, na itasimama katika eneo lake na alitasogea kutoka pale, hulilia, lakini haiwezi kujibu wala kumuokoa yeyote kwenye matatizo.
8 Tafakari kuhusu hivi vitu; katu usivipuuzie, enyi waasi!
9 Tafakari kuhusu vitu vya awali, nyakati zile zilizopita, Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine, Mimi ni Mungu na hakuna kama mimi.
10 Mimi ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya kitu ambacho hakijatokea; Ninasema, ''Mpango wangu utatokea na nitafanya kama ninavyotamani.''
11 Nitamuita ndege wa mawindo kutoka mashariki, Mtu ambaye ni chaguo langu kutoka nchi ya mbali; Ndio nimesema; na pia nitayatimiza haya, nimekusudia, na pia nitafanya hivyo.
12 Nisikilize mimi, enyi watu makaidi, ambao mko mbali na kutenda mema.
13 Ninaileta haki yangu karibu; na wala sio mbali, na wokovu wangu hausubiri; na nitatoa wokovu wangu kwa Sayuni na uzuri wangu kwa Israeli.