61
Roho ya Bwana Yahwe i juu yangu, maana Yahwe amenipaka mafuta mimi kuhiubiri habari njema kwa wenye taabu. Amenituma mimi kuwaponywa waliopondeka mioyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kufungua gereza ili waliofungwa waweze kutoka. Amenituma mimi kuutangaza mwaka wa Yahwe uliokubalika, siku ya kisasi cha Mungu wetu, na kuwafariji wale wote wanaomboleza. Amenituma mimi - kuwapa wale waoombolezao katika Sayuni -kuwapa wao kilemba cha majivu, mafuta ya furaha badala ya kuomboleza, vazi la kusifu katika eneo la roho ya ubutu, kuwaita mialoni ya haki, iliyooteshwa na Yahwe, ili aweze kutukuzwa. Wataijenga tena mahali pa kale palipohaibiwa; wataparejesha mahali palipokuwa na ukiwa. Watairejesha miji iliyoharibiwa, Mahali penye ukiwa kutoka vizazi vingi vilivyopita. Wageni watasimama na kulisha makumdi yako, na watoto wa wageni watafanya kazi kwenye mashamba yako na mizabu. Mtaitwa makuhani wa Yahwe; watawaita watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, na utajivuinia katika utajiri wake. Badala yake aibu yenu itaongezeka; na badala ya fedhea walifurahia juu ya sehemu yao. Hivyo basi sehemu yao itaongezeka mara mbili katika nchi na furaha ya milele itakuwa yao. Maana Mimi, Yahwe, ninapenda haki, na ninachukia wizi na vurugu zisizo za haki. Nitawalipa wao kataka haki na Nitafanya agano la milele na wao. Uzao wao utajulikana miongoni mwa mataifa, na watoto wao miongoni mwa watu. Wote watakaowaona watawakubali wao, kwamba ni watu wangu ambao Yahwe amewabariki. 10 Nitafurahia sana katika Yahwe; Katika Mungu nitafurahia. Maana amenivika mimi kwa vazi la wokovu; amenivika mimi kwa vazi la haki, kama bwana harusi aliyejipamba mwenywe kwa kilemba, na kama bibi harusi aliyejipamba kwa vito. 11 Maana kama nchi inavyozalisha miti inayochipukia na kama bustani inavyofanya miti yake ikuie, hivyo Bwana atasasbabisha haki na sifa kuchipukia mbele ya mataifa yote.