64
1 ''Oh, ikiwa umeigawa kwa kuifungua mbingu na kushuka chini! Milima inetikisika mbele yako,
2 ni kama vile moto uunguzao vichaka, moto uchemshao maji. Oh, jina lako lingejulikana kwa maadui wako, na ya kwamba mataifa yangetetemeka mbele yako!
3 Awali, ulipofanya mambo ya ajabu ambayo hatukuyategemea, ulishuka chini, milima ikatetemeka mbele zako.
4 Tangu nyakati za kale hakuna hata mmoja aliyesikia au kujua, wala jicho kuona Mungu yeyote karibu yake, ni nani afanyae mambo haya kwake anayemsubiri yeye.
5 Umekuja kuwasidia wale wanaofurahia kutenda yaliyo ya haki, wale wanaowaita kuwakumbusha njia zake na kumheshimu yeye. Ulipatwa na hasira tulipotenda dhambi. Katika njia zako daima tutakombolewa.
6 Maana sote tumekuwa kama mmoja aliye na unajisi, na matendo yetu ya haki yamekuwa kama hedhi kali. Sote tumenyauka kama majani; maovu yetu, ni kama upepo, unaotupeperusha sisi mbali.
7 Hakuna hata mmoja anayeita jina lako, hakuna anayefanya jitihada za kukushika wewe; maana umeuficha uso wako mbali na sisi na kutufanya sisi kuwa takataka katika mkono wa maovu yetu.
8 Na lakini, Yahwe, wewe ni baba yetu; sisi ni udongo. Wewe ni mfinyanzi wetu; sisi ni kazi ya mkono wako.
9 Usiwe na hasira kubwa, Yahwe, wala daima usikumbuke maovu dhidi yetu, tafadhali sisi sote, watu wako.
10 Miji yenu mitakatifu imekuwa jangwa; Sayuni imekuwa jangwa, Yerusalemu imekuwa ukiwa.
11 Hekalu letu takatifu na zuri. mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, limeangamizwa kwa moto, na kila kilichokuwa karibu kiliharibiwa.
12 Je unawezaje kuendelea kumshika, Yahwe? Unawezaje kutulia kimya na kuendelea kutufedhehesha sisi?''