26
1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “Mmemsaidiaje aliyedhaifu!
3 Jinsi gani mmemshauri asiye na hekima na kutamka maneno yenye maarifa kwake!
4 Kwa msaada wa nani mmesema maneno haya? Ni roho ya nani iliyotoka ndani yenu?
5 Maiti inatetemeka chini ya maji, na vyote wilivyomo ndani yake.
6 Kuzimu kuko wazi mbele ya Mungu; uharibifu hauna kizuizi dhidi yake.
7 Huitandaza kaskazi juu ya nafasi wazi na kuining'iniza dunia hewani.
8 Huyafunga maji katika mawingu yake mazito, lakini hayagawanyiki chini yake.
9 Huufunika uso wa mwezi na kueneza mawingu yake juu yake.
10 Amechora ukingo wa duara juu ya maji kama mpaka kati ya nuru na giza.
11 Nguzo za mbinguni zinatikisika na zimestushwa na kukemea kwake.
12 Aliituliza bahari kwa uwezo wake; kwa ufahamu wake alimwaribu Rahab
13 Kwa pumzi yake, aliziondoa mbingu kwa dhorubu; mbingu ziliondolewa kwa dhorubu; mkono wake ulimchoma nyoka anayekimbia.
14 Tazama, hizi si zaidi ya madogo ya njia zake; Jinsi gani tunasikia akitunong'oneza! Ni nani awezaye kufahamu uwezo wake.