33
1 Kwahiyo sasa, nakuomba wewe, Ayubu, usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote.
2 Tazama sasa, nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu.
3 Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu; yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua.
4 Roho ya Mungu imeniumba; pumzi ya Mwenye nguvu imenipatia uhai.
5 Kama unaweza, nijibu; weka maneno yako katika mpangilio mbele yangu na kisha usimame.
6 Tazama, niko kama wewe ulivyo mbele za Mungu; nimeumbwa pia kutoka katika udongo.
7 Ona, tishio langu halitakufanya wewe uogope; wala mzigo wangu hautakuwa mzito kwako.
8 Umesema kwa hakika katika masikio yangu; nimeisikia sauti ya maneno yakeo yakisema,
9 'Mimi ni safi na bila hila; sina hatia, na hakuna dhambi ndani yangu.
10 Tazama, Mungu huona nafasi za kunishambulia mimi; huniangalia mimi kama adui yake.
11 Huweka miguu yangu akiba; naye huangalia njia zangu zote.'
12 Tazama, katika hili hauko sawa, nitakujibu, kwa kuwa Mungu ni mkuu kuliko mtu.
13 Kwanini unashindana naye? Huwa hahesabu matendo yake yoyote.
14 Kwa kuwa Mungu huzungumza mara moja, naam, mara mbili, ingawa mwanadamu hawezi kutambua.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani -
16 basi Mungu hufungua masikio ya watu, na kuwatisha kwa vitisho,
17 kwa kusudi la kumvuta mtu atoke katika makusudio yake maovu, na kuyaweka majivuno mbali naye.
18 Mungu huyaokoa maisha ya mwanadamu kutoka katika shimo, na uhai wake dhidi ya kifo.
19 Mtu huadhidibiwa pia na maumivu kitandani mwake, na maumivu makali yanayodumu katika mifupa yake,
20 ili kwamba maisha yake yachukie chakula, na roho yake ichukie vyakula vizuri.
21 Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake, mara moja isionekane, sasa basi ng'ang'ania.
22 Hakika, roho yake inasogea shimoni, na uhai wake unasogea kwa wale wanaotaka kuuharibu.
23 Lakini kama kuna malaika anayeweza kuwa mpatanishi kwa ajili yake, mpatanishi mmoja miongoni mwa maelfu ya malaika, kumwonesha kile kilicho cha haki ili atende haki,
24 na kama malaika ni mpole kwake na kumwambia Mungu, 'Mwokoe mtu huyu ili asishuke chini shimoni; nimepata fidia kwa ajili yake,'
25 kisha mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto, atazirudia siku za nguvu za ujana wake.
26 Atamwomba Mungu, na Mungu atakuwa mwema kwake, ili kwamba auone uso wa Mungu akiwa mwenye furaha. Mungu atampa mtu ushindi wake.
27 Ndipo mtu huyo ataimba mbele ya watu wengine na kusema, 'Nilitenda dhambi na kuasi kile kilichokuwa cha haki, lakini dhambi yangu haikuadhibiwa.
28 Mungu ameiokoa roho yangu isiende chini shimoni; maisha yangu yataendelea kuuona mwanga.'
29 Tazama, Mungu hufanya mambo haya yote pamoja na mwanadamu, mara mbili, naam, hata mara tatu,
30 kuirudisha roho yake kutoka shimoni, ili kwamba aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.
31 Ayubu, zingatia na unisikilize mimi; nyamaza nami nitasema.
32 Ikiwa una kitu cha kusema, na unijibu; sema, maana nataka kuhakikisha kwamba wewe uko katika haki.
33 Kama sivyo, basi nisikilize, ubaki kimya, nami nitakufundisha wewe hekima.”