20
1 Pashuri, mwana wa Imeri, kuhani, alikuwa msimamizi mkuu, akamsikia Yeremia akihubiri maneno haya mbele ya nyumba ya Bwana.
2 Basi Pashuri akampiga nabii Yeremia, akamtia katika masanduku yaliyokuwa kwenye lango la juu la Benyamini ndani ya nyumba ya Bwana.
3 Ikawa siku ya pili Pashuri akamtoa Yeremia nje ya makabati. Yeremia akamwambia, “Bwana hakukuita Pashuri, lakini wewe ni Magor-Misabibu.
4 Kwa maana Bwana asema hivi, 'Tazama, nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wewe na wapendwa wako wote; kwa maana wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona. Nitawatia Yuda mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atawafanya kuwa mateka huko Babeli au kuwaangamiza kwa upanga.
5 Nitampa mali zote za jiji hili na utajiri wake wote, vitu vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Nitaweka vitu hivi mikononi mwa adui zako, nao watawakamata. Nao watawachukua na kuwaleta Babeli.
6 Lakini wewe Pashuri, na wenyeji wote wa nyumba yako watakwenda mateka. Utakwenda Babeli na kufa huko. Wewe na wapendwa wako wote ambao uliwatabiria maneno ya uongo mtazikwa huko.'”
7 “Umenidanganya, Bwana. Kwa hakika nimedanganyika. Wewe ulinikamata na kunishinda. Nimekuwa kitu cha kuchekesha. Watu wananidharau kila siku, siku zote.
8 Kwa maana wakati wowote nimenena, nimeita na kutangaza, 'Vurugu na uharibifu.' Na neno la Bwana limefanywa shutumu na dhihaka kwangu kila siku.
9 Nami nikisema, 'Sitafikiria juu ya Bwana tena. Sitatangaza tena jina lake.' Ni kama moto moyoni mwangu, uliofanyika ndani ya mifupa yangu. Kwa hiyo ninajitahidi kustahimili lakini siwezi.
10 Nimesikia habari za ugaidi kutoka kwa watu wengi pande zote. 'Mshitaki! Lazima tumshitaki' Wale walio karibu nami kuangalia kama nitaanguka. 'Labda anaweza kudanganywa. Ikiwa ndivyo, tunaweza kumshinda na kujilipiza kisasi kwake.'
11 Lakini Bwana yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu, hivyo wale wanaonifuata watajikwaa. Hawatanishinda. Watakuwa na aibu sana, kwa sababu hawatafanikiwa. Watakuwa na aibu ya kudumu, haitasahauliwa kamwe.
12 Lakini wewe, Bwana wa majeshi, wewe unayemtazama wenye haki na ambaye huona akili na moyo. Hebu nipate kuona kisasi chako juu yao kwa maana nimekuletea shitaka langu kwako.
13 Mwimbieni Bwana! Msifuni Bwana! Kwa kuwa ameokoa maisha ya wale waliokandamizwa kutoka kwenye mikono ya waovu.
14 Na ilaaniwe siku niliyozaliwa. Usiruhusu siku ambayo mama yangu alinizaa ibarikiwe.
15 Na alaaniwe mtu aliyemwambia baba yangu akisema, 'Amezaliwa mtoto wa kiume,' na kusababisha furaha kubwa.
16 Mtu huyo atakuwa kama miji ambayo Bwana aliiangamiza bila huruma. Na asikie wito wa msaada asubuhi na sauti ya vita wakati wa mchana.
17 Hiyo itatokea, kwa kuwa Bwana hakuniua tumboni au kumfanya mama yangu kaburi langu, tumbo la ujauzito milele.
18 Kwa nini nilitoka tumboni ili kuona matatizo na uchungu, ili siku zangu zijazwe na aibu?”