34
1 Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yahwe, wakati Nebukadreza mfalme wa Babeli, majeshi yake yote, pamoja na falme zote za dunia, maeneo yote yaliyo chini ya mamlaka yake, na watu wake wote walikuwa wanapigana vita dhidi ya Yerusalemu na miji yake yote, kusema:
2 'Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nenda na uzungumze kwa Sedekia mfalme wa Yuda na useme kwake, 'Yahwe asema hivi: Angalia, niko karibu kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atauchoma moto.
3 Hautapona kutoka mkono wake, kwa maana kwa hakika utakamatwa na kutiwa mkononi mwake. Macho yako yatayaangalia macho ya mfalme wa Babeli; atazungumza kwako moja kwa moja ukiwa unaenda Babeli.'
4 Sedekia mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Yahwe! Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, 'Hautakufa kwa upanga.
5 Utakufa katika amani. Kama kwenye mafukizo ya babu zako, wafalme waliokuwepo kabla yako, watauchoma mwili wako. Watasema, 'Ole, bwana!” Watakuomboleza. Sasa nimesema—hili ni tangazo la Yahwe.”
6 Kwa hiyo Yeremia nabii akatangaza kwa Sedekia mfalme wa Yuda maneno haya yote katika Yerusalemu.
7 Jeshi la mfalme wa Babeli likafanya dhidi ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda iliyobaki: Lakishi, na Azeka. Miji hii ya yuda ilisalia kama miji yenye maboma.
8 Neno lilomjia Yeremia kutoka kwa Yahwe baada ya mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote katika Yurusalemu, ili kuwatanagazia uhuru
9 ya kwamba kila mtu lazima amwachie huru mtumwa wake wa Kiebrania, wote wa kiume na wa kike, kwa hiyo mtu alipaswa kutomtumikisha Myahudi, ambaye alikuwa ndugu yake.
10 Kwa hiyo watu wote na viongozi wakaingia katika agano kwamba kila mtu amwachie huru mtumwa wake wa kiume na waikke ili asiwe mtumwa tena. Walitii na kuwaweka huru.
11 Lakini baada ya hapo walibadili akili zao. Wakawarudisha watumwa ambao walikuwa wamewaachia huru. Wakawalazimisha kuwa wataumwa tena.
12 Kwa hiyo neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
13 “Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Mimi mwenyewe nilifanya agano na babu zenu katika siku ambayo niliwatoa nje ya nchi ya Misiri, nje ya nyumba ya utumwa. Hapo ndipo niliposema,
14 Katika mwisho wa mwaka wa saba, kila mtu lazima amwachie ndugu yake, Mwebrania mwenzake aliyejiuza mwenyewe kwako ili kukutumikia kwa miaka sita. Mwagize aende kwa uhuru.” Lakini babu zenu hawakunisikiliza wala kutega masikio yao kwangu.
15 Sasa ninyi wenyewe mlitubu na kuanza yaliyomema katika macho yangu. Mlitangaza uhuru, kila mtu kwa jirani yake, na mlifanya agano mbele zangu kwenye nyumba iitwayo kwa jina langu.
16 Lakini tena mmegeuka na kulichafua jina langu; mmemsababisha kila mtu kumleta tena mtumwa wake wa kiume na wa kike, wale mliowachie kwenda walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa tena.'
17 Kwa hiyo Yahwe asema hivi, 'Ninyi wenyewe hamkunisikiliza. Mlipaswa kuwa mmetangaza uhuru, kila mmoja wenu, kwa ndugu zenu na Waisraeli wenzenu. Kwa hiyo angalia! Niko karibu kutangaza uhuru kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—uhuru wa upanga, tauni, na njaa, kwa maana naenda kuwafanya kitu cha ajabu katika macho aya kila ufalme juu ya dunia.
18 Kisha nitashughulika na watu waliolivuja agano langu, ambao hawakuyashika maneno ya agano ambalo walilithibitisha mbele zangu walipomkata ng'ombe dume katika vipande viwili na kutembea katika vipande vyake,
19 na kisha viongozi wa Yuda na Yerusalemu, matowashi na makuhani, na watu wote wa nchi wakatembea katika vipande vya yule ng'ombe dume.
20 Nitawatia katika mikono ya adui zao na katika mikono ya hao wanaoutafuta uhai wao. Miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama juu ya dunia.
21 Kwa hiyo nitawatia Sedekia mfalme wa Yuda na viongozi wake kwenye mikono ya adui zao na kwenye miko ya wale wanaoutafuta uhai wao na katika mikono ya majeshi ya mfalme wa Babeli ambayo yameinuka dhidi yenu.
22 Angalia, niko karibu kutoa amari—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawaleta tena kwenye mji huu ili wapigane dhidi yake, na kuunguza kwa moto. Kwa maana nitaigeuza miji ya Yuda kuwa sehemu za ukiwa ambamo hapatakuwa na wakaaji.”