41
1 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmael mwana wa Nethania mwana wa Elishama, toka familia ya kifalme, na maafisa baadhi wa mfalme, walikuja - wanaume kumi walikuwa pamoja naye - kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpa. Walikula chakula pamoja hukp Mizpa.
2 Lakini Ishmael mwana wa Nethania, na wanaume kumi ambao walikuwa pamoja naye waliinuka na kumvamia Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, kwa upanga. Ishmael alimuua Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alimweka kuwa msimamizi wa nchi.
3 Kisha Ishmael aliwauwa Wayahudi wote ambao walikuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na Wakaldayo wanaume wa kupigana kukutwa huko.
4 Kisha ilikuwa siku ya pili baada ya kumuua Gedila, lakini hakuna moja aliyejua.
5 Wanaume baadhi walikuja toka Shechem, toka Shiloh, na toka Samaria-wanaume semanini ambayo walikuwa wamenyoa ndevu zao, walirarua nguo zao, na kujikata wenyewe- pamoja na chakula cha sadaka na ubani katika mikono yao kwenda kwa nyumba ya Yahwe.
6 Basi Ishmael mwana wa Nethania alienda toka Mizpa kukutana nao kama walivyoenda, wakitembea na kulia. Kisha ilitokea kwamba kama alivyokutana nao, alisema nao, “Njoo kwa Gedalia mwana wa Ahikam!”
7 Ilikuja kuwa kwamba wakati walipokuja katika mji, Ishmaeil mwana wa Nethania aliwauwa na kuwatupa kwenye shimo, yeye na wanaume ambao walikuwa pamoja naye.
8 Lakini palikuwa na wanaume kumi miongoni mwao ambao walisema kwa Ishmael, “ Usituue, kwa kuwa kuna riziki zetu kwenye shamba: ngano na shayiri, mafuta na asili” Kwa hiyo hakuwauwa pamoja na rafiki zao wengine.
9 Kisima ambacho Ishmael alitupa miili yote ya waliokufa ambaye yeye na Gedalia waliwapiga, kilikuwa ni kilekile ambacho mfalme Asa alichimba wakati alipokuwa akivamiwa na mfalme Baasha wa Israel. Ishmael mwana wa Nethania alilijaza wale ambao walikuwa wameuawa.
10 Badae Ishmael aliwashika watu wengine wote ambao walikuwa huko Mizpa, mabinti wa mfalme na watu wote ambao walikuwa wameachwa huko Mizpa ambayo Nebuzaradani mlinzi mkuu alikuwa amewakabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikam. Basi Ishmael mwana wa Nethania aliwashika na kuvuka kwa watu wa Ammon.
11 Lakini Yonathani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi pamoja naye walisikia madhara yote ambayo Ishmael mwana wa Nethania alikuwa amefanya.
12 Basi waliwachukua wanaume wao na kwenda kupigana dhidi ya Ishmanel mwana wa Nethania. Walipigana naye huko kwenye kisima kuu cha Gibeoni.
13 Kisha ilitokea kwamba wakati watu wote ambao walikuwa na Ishmael kuona Yonathani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi ambao walikuwa pamoja naye, walikuwa na furaha.
14 Basi watu wote ambao Ishmael alikuwa amewashika huko Mizpa waligeuka na kwenda kwa Yonathani mwana wa Karea.
15 Lakini Ishmael mwana wa Nethania alitoroka na wanaume wanane toka kwa Yonathani. Alienda kwa watu wa Ammon.
16 Yonathani mwana wa Karea na amri jeshi pamoja naye walichukua toka Mizpa watu wote ambao walikuwa wameokolewa kutoka kwa Ishmael mwana wa Nethania. Hii ilikuwa baada ya Ishmael kuwa amemuuwa Gedalia mwana wa Ahikam. Yonathan na rafiki zake walichukua wanaume shujaa, wanaume wapiganaji, wanawake na watoto, na mtoashi ambaye alikuwa ameokolewa huko Gibeoni.
17 Kisha walienda na kubaki kwa muda huko Geruthi Chimham, ambayo iko karibu Bethelemu. Walikuwa wakienda Misri
18 kwa sababu ya Wakaldayo. Walikuwa wakiwaogopa kwani Ishmael mwana wa Nethania alikuwa amemua Gedalia mwana wa Ahikam, ambaye mfamle wa Babeli amewekwa kwenye usimamizi wa nchi.