7
1 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Yermia,
2 Simama katika lango la nyumba ya BWANA na utangaze ujumbe huu! Sikiilizeni neno la BWANA, ninyi nyote watu wa Yuda, ninyi mnaoingia katika malango haya kumwabudu BWANA.
3 BWANA wsa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Tengenezeni njia zenu na kufanya mema, nami nitawaacha muishi hapa.
4 Msitumainie maneno ya uongo mkisema, “Hekalu la BWANA!, Hekalu la BWANA! Hekalu la BWANA!”
5 Bali kama mtazitengeneza njia zenu na kufanya mema, kama mtatoa hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake
6 -kama hamtanyonya anayekaa katika nchi, yatima, mjane, na kama hamtamwaga damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa, na kama hataenda kwa miungu mingine kwa ajili ya maumivu yenu
7 -ndipo nitakapowaacha mkae mahali hapa, katika nchi ambayo niliwapia mababu zenu toka zamani na hata milele.
8 Tazama! Mnatumainia maneno ya uongo ambayo hayawasaidii.
9 Je, mnaiba. mnaua, manafanya uzinzi? na mnaapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kwenda kwa miungu mingine ambao hamkuwajua?
10 Je, mnakuja na kusimama mbele yangu katika nyumba hii ambapo jina langu linatangazwa na kusema, “Tumeokoka.” hivyo mnaweza kufanya machukizo yote haya?
11 Je, hii ndiyo nyumba inayobeba jina langu, pango la wanyang'anyi mbele ya macho yenu? Lakini tazama, Nimeiona - BWANA asema.'
12 Kwa hiyo uende mahali pangu kule Shiloh, Kule ambako mwanzoni niliruhusu jina langu kukaa, na tazama kile nilichofanya pale kwa sababu ya maovu ya watu wangu Israeli.
13 Kwa hiyo sasa, kwa sababu ya matendo yako haya yote - asema BWANA - Nilikuambia mara kadhaa, lakini hukusikiliza. Nilikuita, lakini hukuitika.
14 Kwa hiyo kile nilichofanya Shilo, ndicho ambacho pia nitakachofanya kwa nyumba yangu hii inayoitwa kwa jina langu, nyumba amabyo ninyi mmeitumainia, mahali hapa ambapo niliwapa ninyi na mababu zenu.
15 Kwa kuwa nitawafukuza mtoke kwangu kama vile nilivyowafukuza ndugu zenu wote, uzao wote wa Efraimu.'
16 Na wewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa, na usiinue maombolezo ya kilio au kuomba sala kwa niaba yao, na usinishi, kwa kuwa sitakusikiliza.
17 Kwani huoni kile wanachofanya katika miji ya Yuda na katika mitaa ya Yerusalemu?
18 Watoto wanakusanya kuni na baba zao huwasha moto! Wanawake hukanda unga ili kuoka mikate kwa ajili ya malikia wa mbinguni na kumimina sadaka ya vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha mimi.
19 Ni kweli wananikasirisha mimi? - asema BWANA - Je, si wao wanaojikasirisha, ili kwamba aibu iwe juu yao?
20 Kwa hiyo BWANA, Mungu asema hivi, 'Tazama, hasira na ghahdabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, kwa watu wote na wanyama, juu ya miti katika mashamba na mazao ya ardhi, Itawaka nayo haitazimishwa.
21 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Jiongezeeni sadaka za kuteketezwa katika dhabihu zenu na nyama zake.
22 Kwani wakati nilipowatoa mababu zenu kutoka nchi ya Misri, Sikuhitaji chochote kutoka kwao. Sikuwapa amri juu ya maswala ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu.
23 Niliwapa amri hii tu, “Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Kwa hiyo muishi katika njia ambazo ninawaamuru, ili mambo yenu yawe mazuri.”
24 Lakini hawkunisikiliza wala kuzingatia. Walishi kwa kufuata mipango yao ya uasi ya mioyo ya maovu, kwa hiyo walirudi nyuma badala ya kuendelea mbele.
25 Tangu siku ambayo mababu zenu walitoka katika nchi ya Misri mpaka leo, Nimetuma watumishi wangu, manabii wangu, kwenu. Niliendelea kuwatuma.
26 Lakini hawakuwasikiliza. Hawakuzingatia. Badala yake walishupaza shingo zao. Walikuwa waovu zaidi ya mababu zao.
27 Kwa hiyo yatangaze maneno haya yote kwao, japo hawatakusikiliza. Yatangaze mambo haya kwao, lakini hawatakujibu.
28 Waambie kuwa hili ni taifa ambalo haliisikilizi sauti ya BWANA, Mungu wake na lisilopokea mafundisho. Ukweli uneharibiwa na kukatwa kutoka kwenye vinywa vyao.
29 Zikate nywele zako na kujinyoa, na kuzitupa. Imba wimbo wa maombolezo katika maeneo yaliyo wazi. Kwa kuwa BWANA amekikataa na kukitupa kizazi hiki cha hasira yake.
30 Kwa kuwa wana wa Yuda wamefanya maovu mbele ya macho yangu - asema BWANA - wameweka machukizo yao katika nyumba ambayo jina langu hunenwa, ili kulinajisi.
31 Kisha wamejenga mahali palipoinuka pa Tofethi ambapo pako kwenye bonde la Ben Hinomu. Walifanya hivi ili kuwachoma wana na binti zao kwenye moto - kitu ambacho mimi sikuamuru, wala kuweka jambo hilo katika akili zangu.
32 Kwa hiyo, tazama siku zinakuja - asema BWANA - ambapo hapataitwa tena Tofethi au bonde la Ben Hinomu. Litakuwa bonde la machinjio; watazika maiti hapo Tofethi mpaka eneo lote lienee.
33 Mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa duniani, na hakutakuwa na mtu wa kuwafukuza.
34 Nitazikomesha katika miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalaemu sauti za kuiniuliwa na vicheko, Sauti ya bwana arusi na ya bibi arusi; kwa kuwa nchi hiyo itakuwa ukiwa.”