5
1 Basi Naamani, amri jeshi wa mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa na mtu mwenye kuheshimiwa mbele ya bwana wake, kwa sababu kwa ajili yake Yahwe aliwapa ushindi Washami. Pia alikuwa hodari, mtu shujaa, lakini alikuwa anaukoma.
2 Washami walikuwa wametoka kuongoza kikosi na kumchukua kijana mdogo wa kike kutoka nchi ya Israeli. Akamuhudumia mke wa Naamani.
3 Yule binti akamwambia bibi yake, “Natamani kwamba bwana wangu angelikuwa na nabii ambaye yupo Samaria! Halafu angelimponya bwana wangu ukoma wake.
4 Hivyo Naamani akaingia na kumwambia mfalme kile ambacho yule binti kutoka nchi ya Israeli alichokuwa amekisechosema.
5 Kisha mfalme wa Shamu akase, “Nenda sasa, na nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Naamani akaondoka na kuchukua talanta zake kumi za fedha, vipande elfu sita vya dhahabu, na nguo kumi za kubadilisha.
6 Pia alichukua barua ya kumpelekea mfalme wa Israeli inayosema, “Sasa wakati hii barua itakapoletwa kwako, utaona kwamba nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, hivyo basi utamponya ukoma wake.”
7 Wakati mfalme wa Israeli alipoisoma ile barua, alichana mavazi yake na kusema, “Je mimi ni Mungu, niue na nirudishe uhai, kwamba huyu mtu anataka nimponye mtu ukoma wake? Inaonekana anatafuta mashindano na mimi.”
8 Ikawa wakati Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alichana nguo zake, akatuma neno kwa mfalme akisema, “Kwa nini umechana nguo zako? Muache aje kwangu sasa, na atajua kwamba kuna nabii katika Israeli.”
9 Basi Naamani akaja na farasi wake na mikokoteni yake ya kukokotwa na farasi na kusimama kwenye mlango wa nyumba ya Elisha.
10 Elisha akamtumia mjumbe, akisema, “Nenda na ukazame mwenyewe katika Yordani mara saba, na ngozi ya mwili wako itajirudi; utakuwa msafi.”
11 Lakini Naamani alikasirika na kuondoka na kusema, “Tazama, Nilidhani bila shaka angekuja kwangu na kusimama na kuliita jina la Yahwe Mungu wake, na kupitisha mkono wake kwenye sehemu ya ugonjwa na kuponya ukoma wangu.
12 Je sio Abana na Faepari, mito ya Damaskasi, bora kuliko maji yote ya Israeli?” Je siwezi kuoga ndani yao na kuwa safi?” Hivyo akageuka na kwenda kwa hasira.
13 Ndipo watumishi wa Naamani wakaja karibbu na kumwambia, “Baba yangu, kama yule nabii alikuamuru kufanya kitu kigumu, singelifanya? Je si zaidi basi, atakapokwambia rahisi, 'Zama mwenyewe na uwe safi?”
14 Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili ya mtoto mdogo, na alikuwa amepona.
15 Naamani akarudi kwa yule mtu wa Mungu, yeye na watu wake wengine, na kuja na kusimama mbele yake. Akasema, “Tazama, sasa najua kwamba hakuna Mungu katika Dunia nzima isipokuwa katika Israeli. Kwa hiyo basi, chukua zawadi kutoka kwa mtumishi wako tafadhali.”
16 Lakini Elisha akajibu, “Kama Yahwe aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sintopokea chochote.”Naamani akamsihi Elisha apokee zawadi, lakini alikataa.
17 Hivyo Naamani akasema, “Kama sivyo, nakuomba ache apewe mtumishi wako pale mzigo wa baghala mbili za aridhi, kwa kuwa kuanzia sasa, mtumishi wako hatotoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa mungu yeyote isipokuwa Yahwe.
18 Katika jambo hili moja Yahwe anaweza kumsamehe mtumishi wako, hii ni, wakati mfalme wangu atakapoenda kwenye nyumba ya Rimoni kuabudu pale, na kujifunza kwenye mikono yangu na kumuinamia mwenyewe kwenye nyumba ya Rimoni, Yahwe aweze kumsamehe mtumishi wako katika hili jambo.”
19 Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.” Hivyo Naamani akaondoka.
20 Alikuwa amesafiri lakini umbali mfupi, wakati Gehazi mtumishi wa Elisha mtumishi wa Mungu alisema mwenyewe, “Tazama, bwana wangu amemuandaa huyu Naamani Mshami kwa kuacha kupokea zawadi kutoka kwenye mikono yake ambazo alizileta. Kama Yahwe aishivyo, Nitakimbia nikimfuata na kupokea kitu kutoka kwake.
21 Hivyo Gehazi akamfuata Naamani. Wakati Naamani alipomuona mtu mmoja anakimbia akimfuata, aliruka chini kutoka kwenye gari yake kuonana naye na kusema, “Je kila kitu kiko sawa?”
22 Gehazi akasema, “kila kitu kiko sawa. Bwana wangu amenituma, akisema, 'Tazama, sasa wamekuja kwangu kutoka nchi ya mlima ya Efraimu vijana wawili wa watoto wa manabii. Tafadhali, wapatie talanta ya fedha na nguo mbili za kubadilisha.”
23 Naamani akajibu, “Ninafuraha kubwa kukupatia talanta mbili.” Naamani akamsihi Gehazi na kujaribu talanta mbili za fedha kwenye mifuko miwili ya kubebea, pamoja na nguo mbili za kubadilisha, na kutandaza kwa wafanyakazi wake wawili, ambao walikuwa wamebebea ile mifuko miwili ya fedha mbele ya Gehazi.
24 Wakati Gehazi alipokuja kwenye ule mlima, alichukua ile mifuko ya fedha kutoka kwenye mikono yao na kuificha kwenye nyumba; akawatuma wale watu, na wakaondoka.
25 Wakati Gehazi alipoingia na kusimama mbele ya bwana wake, Elisha akamwambia, “Umetokea wapi, Gehazi?” Akajibu, “Mtumishi wako hakwenda mahali.”
26 Elisha akamwambia Gehazi, “Je roho yangu haikuwa na wewe wakati yule mtu alipoyarudisha magari yake ya farasi ili kukutana na wewe? Je uu ni mda wa kupokea pesa na nguo, mashamba ya mzaituni na mizabibu, na kondoo na Ng'ombe, na watumishi wakiume na watumishi wakike?
27 Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima.” Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.