6
1 Sasa sikilizeni kile ambacho Yahwe asemacho, “Inuka na ueleze kesi yako mbele ya milima; acha milima isikie sauti yako.
2 Sikilizeni madai ya Yahwe, enyi milima, na ninyi misingi mivumilivu ya dunia. Kwa kuwa Yahwe anavumilia pamoja na watu wake, na atapigana katika mahakama juu ya Israeli.”
3 Watu wangu, nimefanya nini kwenu? nimewachosha mara ngapi? shuhudieni dhidi yangu!
4 Kwa kuwa niliwaleta kutoka nchi ya Msiri na kuwaokoa kutoka kwenye nyumba ya utumwa. Nawatuma Musa, Aruni, na Mariamu kwako.
5 Watu wangu, kumbukeni ambavyo Balaki mfalme wa Moabu alivyotunga, na vile ambavyo Balamu mwana wa Beori alivyomjibu kama ulipokuwa ukienda kutoka kwa Gilgali, hivyo mnaweza kujua matendo ya haki ya Yahwe.”
6 Je nilete nini kwa Yahwe, ninapoenda kumwinamia Mungu aliye juu? Je ninaweza kuja kwake na sadaka za kuteketeza, pamoja na ndama wenye mwaka mmoja?
7 Je Yahwe atapendezwa na maelfu ya kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, tunda la mwili wangu kwa ajili ya dhambi yangu mwenyewe?
8 Amekwambia, mtu, kile kilicho bora, na kile ambacho Yahwe atakacho kutoka kwako: Kutenda haki, kupenda ukarimu, na kutembea kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wako.
9 Sauti ya Yahwe inatangaza kwenye mji-hata sasa hekima hukukiri jina lako: “Kaa tayari kwa ajili ya fimbo, na kwa yule aliyeiweka.
10 Kuna utajiri katika nyumba za waovu, na kipimo cha uongo hilo ni chukizo mno.
11 Ningeweza kumfikira mtu kuwa hana hatia kama anatumia kipimo cha ulaghai, pamoja na mfuko wa kipimo wa udanganyifu?
12 Matajiri wamejaa uharibifu, makazi yao yamesema uongo, na ulimi wao katika midomo yao unaudanganyifu.
13 Kwa hiyo nimekupiga kwa pigo linaloumiza, nimekufanya gofu kwa sababu ya dhambi zako.
14 Utakula lakini hutatosheka; utupu wako utabakia ndani yako. Utatunza mizigo mbali lakini hutahifadhi, na kile unachokihifadhi nitakitoa kwa upanga.
15 Utapanda lakini huatavuna; utazikusanya zaituni lakini hutajipaka mafuta; utasindika zabibu lakini hutakunywa divai.
16 Kanuni zilizotengenezwa na Omri zimetunzwa, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu. Mnatembea kwa ushauri wao. Hivyo nitakufanya wewe, mji, gofu, na makazi yako jambo la zomeo, na matabeba dharau kama watu wangu.”