14
1 Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu..
2 Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.”
3 Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.
4 Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.”
5 Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.
6 Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode.
7 Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.
8 Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
9 Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike.
10 Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani
11 ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake.
12 Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.
13 Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.
14 Kisha Yesu alikuja mbele yao akauona umati mkubwa. Akawaonea huruma na kuponya magonjwa yao.
15 Jioni ilipotimia, wanafunzi wakaja kwake na kusema, “Hii ni sehemu ya jangwa, na siku tayari imepita. Watawanyishe makutano ili waende vijijini wakanunue chakula kwa ajili yao.
16 Lakini Yesu akawaambia, ''Hawana haja ya kwenda zao. Wapeni ninyi chakula”
17 Wakamwambia, ''Hapa tunayo mikate mitano na samaki wawili tu.”''
18 Yesu akasema, “Ileteni kwangu.”
19 Kisha Yesu akauamuru umati kukaa chini ya nyasi. Akachukuwa mikate mitano na samaki wawili. Akatazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate akawapa wanafunzi. Wanafunzi wakaupatia umati.
20 Wakala wote na kushiba. Kisha wakavikusanya vipande vyote vya chakula na kujaza vikapu kumi na mbili.
21 Wale waliokula walikadiriwa kuwa wanaume elfu tano bila ya kusehabu wanawake na watoto.
22 Mara moja aliwaamuru wanafunzi waingie ndani ya mashua, wakati huo yeye akawaaga umati waende zao.
23 Baada ya kuwaaga umati kwenda zao, akapanda juu mlimani kuomba pekee yake. Wakati ilipokuwa jioni alikuwa huko pekee yake.
24 Lakini sasa mashua ilipokuwa katikati ya bahari ukiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi, kwani upepo ulikuwa wa mpisho.
25 Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.
26 Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, “Ni mzuka,'' na kupaaza sauti katika hali ya uoga.
27 Yesu akawaambia mara moja, akisema, “Jipeni moyo! ni mimi! msiogope.”
28 Petro alimjibu kwa kusema, “Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.''
29 Yesu akasema, “Njoo.'' Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.
30 Lakini Petro alipoona mawimbi, aliogopa, na kuanza kuzama, chini, akaita sauti na kusema, “Bwana, niokoe!''
31 Haraka Yesu akanyoosha mkono wake akamnyanyua Petro, na kumwambia, “Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini ulikuwa na mashaka?”
32 Ndipo Yesu na Petro walipoingia katika mashua, upepo ulikoma kuvuma.
33 Wanafunzi mashuani wakamwabudu Yesu na kusema, “Kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”
34 Na walipokwisha kuvuka, walifika katika nchi ya Genesareti.
35 Na watu katika eneo lile walipomtambua Yesu, walituma ujumbe kila sehemu za kando, na kuleta kila aliyekuwa mgonjwa.
36 Walimsihi kwamba waweze kugusha pindo la vazi lake, na wengi walioligusa waliponywa.