1 Petro
1
1 Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wageni wa utawanyiko, kwa wateule, katika Ponto yote, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia,
2 kutokana na ufahamu wa Mungu, Baba, kwa kutakaswa na Roho Mtakatifu, kwa utiifu wa Yesu Kristo, na kwa kunyunyuziwa damu yake. Neema iwe kwenu, na amani yenu iongezeke.
3 Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na abarikiwe. Katika ukuu wa rehema yake, alitupa kuzaliwa upya kwa ujasiri wa urithi kupitia ufufuo wa Yesu Kristo kutoka katika wafu,
4 kwa urithi usioangamia, hautakua na uchafu wala kupungua. Umehihifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu.
5 Kwa uwezo wa Mungu mnalindwa kupitia imani kwa wokovu ambao upo tayari kufunuliwa katika nyakati za mwisho.
6 Furahini katika hili, ingawaje sasa ni lazima kwenu kujisikia huzuni katika majaribu ya aina mbalimbali.
7 Hii, ni kwa sababu imani yenu iweze kujaribiwa, imani ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ambayo inapotea katika moto ambao hujaribu imani yenu. Hii hutokea ili imani yenu ipate kuzaa sifa, utukufu, na heshima katika ufunuo wa Yesu Kristo.
8 Hamjamuona yeye, lakini mnampenda. Hamumuoni sasa, lakini mnaamini katika yeye na mna furaha isiyoweza kuelezeka kwa furaha ambayo imejawa na utukufu.
9 Sasa mnapokea wenyewe matokeo ya imani yenu, wokovu wa nafsi zenu.
10 Manabii walitafuta na kuuliza kwa umakini kuhusu wokovu huu, kuhusu neema ambayo ingekuwa yenu.
11 Walitafuta kujua ni aina gani ya wokovu ambao ungekuja. Walitafuta pia kujua ni muda gani Roho wa Kristo aliye ndani yao alikuwa anazungumza nini nao. Hii ilikua inatokea wakati alipokuwa anawaambia mapema kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ambao ungemfuata.
12 Ilifunuliwa kwa manabii kwamba walikua wanayatumikia mambo haya, na si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu - masimulizi ya mambo haya kupitia wale wanaoleta injili kwenu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, mambo ambayo hata malaika wanatamani kufunuliwa kwake.
13 Kwa hiyo fungeni viuno vya akili zenu. Muwe watulivu katika fikra zenu. Muwe na ujasiri mkamilifu katika neema ambayo italetwa kwenu wakati wa kufunuliwa kwa Yesu Kristo.
14 Kama watoto watiifu, msifungwe wenyewe na tamaa ambazo mlizifuata wakati mlipokua hamna ufahamu.
15 Lakini kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi, pia, muwe watakatifu katika tabia yenu yote maishani.
16 Kwa kuwa imeandkwa, “Iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu.”
17 Na kama mkiita “Baba” yule ahukumuye kwa haki kulingana na kazi ya kila mtu, tumia muda wa safari yako katika unyenyekevu.
18 Mnafahamu kwamba haikuwa kwa fedha au dhahabu - vitu vinavyoharibika- ambavyo mmekombolewa kutoka kwenye tabia zenu za ujinga ambazo mlijifunza kutoka kwa baba zenu.
19 Lakini mmekombolewa kwa damu ya heshima ya Kristo, kama ya kondoo asiye na hila wala doa.
20 Kristo alichaguliwa kabla ya misingi ya dunia, lakini sasa siku hizi za mwisho, amefunuliwa kwenu.
21 Mnamwamini Mungu kupitia yeye, ambaye Mungu alimfufua toka kwa wafu na ambaye alimpa utukufu ili kwamba imani yenu na ujasiri uwe katika Mungu.
22 Mmefanya nafsi zenu kuwa safi kwa utii wa ile kweli, kwa dhumuni la pendo la kidugu lililo na unyofu, hivyo pendaneni kwa bidii toka moyoni.
23 Mmekwisha zaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, lakini kutoka katika mbegu isiyoharibika, kupitia uzima na neno la Mungu lililosalia.
24 Kwa maana “ miili yote ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la jani. Jani hunyauka, na ua hudondoka,
25 lakini neno la Bwana hubakia milele.” Huu ni ujumbe ambao ulitangazwa kama injili kwenu.