4
1 Kwa hiyo wapendwa wangu, ambao nawatamani, ambao ni furaha na taji yangu. Simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa.
2 Ninakusihi wewe Eudia, pia ninakusihi wewe Sintike, mrejeshe mahusiano ya amani kati yenu, kwa sababu ninyi, nyote wawili mliungana na Bwana.
3 Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
4 katika Bwana siku zote. tena nitasema, furahini.
5 Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.
6 Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.
7 Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.
8 Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.
9 Yatekelezeni mambo yale mliojifunza, mliyopokea mliyoyasikia na yale mliyoyaona kwangu naye Baba yetu wa amani atakuwa nanyi.
10 Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.
11 Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.
12 Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji.
13 Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
14 Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.
15 Ninyi wafilipi mnafahamu kwamba mwanzo wa injili nilipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi pekee yenu.
16 Hata nilipokuwa Thesaslonika, ninyi mlinitumia msaada zaidi ya mara moja kwa ajili ya mahitaji yangu.
17 Simaanishi kwamba natafuta msaada. Bali nasema ili mpate matunda yaletayo faida kwenu.
18 Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi. Nimepokea vitu vyenu kutoka kwa Epafradito. Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithiri ya manukato, vyenye kukubalika ambavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu.
19 Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.
20 Sasa kwa Mungu na Baba yetu uwe utukufu milele na milele. Amina.
21 Salamu zangu zimfikie kila muumini katika Kristo Yesu. Wapendwa nilio nao hapa wanawasalimieni.
22 Pia waumini wote hapa wanawasalimieni, hususani wale wa familia ya Kaisari.
23 Na sasa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu.