20
Divai ni dhihaka na kinywaji kikali ni mgomvi; anayepotea kwa kunywa hana busara. Kumwogopa mfalme ni kama kumwogopa simba kijana aungurumaye, yeyote anayemkasirisha hutoa fidia ya maish yake. Ni heshima kwa mtu yeyote kujiepusha na mafarakano, bali kila mpumbavu hurukia kwenye mabishano. Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu. Makusudi ndani ya moyo wa mtu ni kama maji yenye kina, bali mtu mwenye ufahamu huyateka. Mara nyingi mtu husema yeye ni mwaminifu, lakini ni nani awezaye kumpata yule mwaminifu? Mtu atendaye haki hutembea katika uaminifu wake na wana wake wanaofuata baada yake wanafuraha. Mfalme anayeketi kwenye kiti cha hukumu akifanya kazi za kuhukumu hupembua kwa macho yake mabaya yote yaliyoko mbele yake. Nani anayeweza kusema, “Nimeuweka safi moyo wangu; nipo huru na dhambi zangu”? 10 Mizani tofauti na vipimo visivyosawa - Yehova huvichukia vyote. 11 Hata kijana hujulikana kwa matendo yake, kwa mwenendo wake kama ni safi na uadilifu. 12 Masikio yanayosikia na macho yanayoona- Yehova aliyafanya yote. 13 Usipende usingizi au utakuwa masikini; fumbua macho yako na utakuwa na vyakula tele. 14 “Mbaya! Mbaya!” anasema mnunuzi, lakini akiondoka anajisifu. 15 Ipo dhahabu na mawe ya thamani, lakini midomo yenye maarifa ni kito cha thamani. 16 Chukua vazi kama mmiliki wake ataweka fedha kama dhamana kwa deni la mgeni, na lichukue kama anaweka dhamana kwa uzinifu. 17 Mkate uliopatikana kwa ulaghai unaladha tamu, lakini baadaye kinywa chake kitajaa kokoto. 18 Mipango huimarishwa kwa ushauri na kwa mwongozo wa busara utapigana vita. 19 Mmbea hufunua siri na kwa hiyo hupaswi kushirikiana na watu ambao huongea sana. 20 Kama mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itapulizwa katikati ya giza. 21 Urithi uliopatikana mwanzoni kwa haraka utakuwa na mema kidogo mwishoni. 22 Usiseme “ Mimi nitakulipiza kwa kosa hili” Msubiri Yehova na yeye atakuokoa. 23 Yehova huchukia mizani isiyo sawa na vipimo vya udanganyifu si vizuri. 24 Hatua za mtu huongozwa na Yehova; namna gani basi ataifahamu njia yake? 25 Ni mtego kwa mtu kusema kwa pupa, “ Kitu hiki ni kitakatifu” na kuanza kufikiri juu yake kwamba kina maana gani baada ya kufanya kiapo. 26 Mfalme mwenye busara huwapepeta waovu na huligeuza juu yao gurudumu la kupuria. 27 Roho ya mtu ni taa ya Yehova, hutafiti sehemu zake zote za ndani kabisa. 28 Agano la uaminifu na udhamini humhifadhi mfalme; kiti chake cha enzi hufanywa thabiti kwa upendo. 29 Utukufu wa watu vijana ni nguvu zao na fahari ya watu wazee ni mvi zao. 30 Mapigo yanayoleta kidonda huusafisha ubaya na vichapo hufanya sehemu za ndani kabisa kuwa safi.