11
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi.
1 Ni kwako Yahweh ninapata usalama; ni kwa namna gani utasema na mimi, “Ruka kama ndege hadi mlimani”?
2 Tazama! Waovu wana andaa pinde zao. Wana tayarisha gizani mishale yao kwenye kamba ili kufyatua mioyo ya wenye haki.
3 Ikiwa misingi imeharibiwa, mwenye haki atafanya nini?
4 Yahweh yuko katika hekalu takatifu; macho yake yanatazama, yakiuchunguza ubinadamu.
5 Yahweh huwachunguza wote wenye haki na waovu, bali huwachukia wapendao kuwaumiza wengine.
6 Yeye huwanyeshea waovu makaa ya mawe na moto wa jehanamu; upepo uunguzao utakuwa ni sehemu yao kutoka katika kikombe chake!
7 Kwa kuwa Yahweh ni mwenye haki, Naye hupenda haki; wenye haki watauona uso wake.