114
1 Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni,
2 Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli.
3 Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma.
4 Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo.
5 Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma?
6 Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo?
7 Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo.
8 Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem.