13
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi.
1 Mpaka lini, Yahweh, utaendelea kunisahau? Ni kwa muda gani utauficha uso wako nisiuone?
2 Ni kwa muda gani nitalazimika kuhofu na kuhuzunika moyoni mwangu kila siku? Ni kwa muda gani adui zangu watanishida?
3 Unitazame na unijibu, Yahwe Mungu wangu! Nipe mwanga machoni pangu, vinginevyo nitalala katika mauti.
4 Usimuache adui yangu aseme, “Nimemshinda huyu,” ili kwamba asiweze kusema, “Nimemtawala adui yangu;” la sivyo, maadui zangu watafurahia nitakapo shushwa chini.
5 Lakini nimeamini katika uaminifu wa agano lako; moyo wangu wafurahia katika wokovu wako.
6 Nitamuimbia Yahwe kwa kuwa ameniganga kwa ukarimu kabisa.