147
1 Msifuni Yahwe, kwa maana ni vyema kumwimbia sifa Mungu wetu, ni kuzuri, kusifu kwa faa sana.
2 Yahwe huijenga tena Yerusalemu, huwakusanya pamoja watu wa Israeli waliotawanyika.
3 Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.
4 Huzihesabu nyota, naye huzipa majina zote.
5 Ukuu ni wa Bwana wetu na nguvu zake ni za kutisha, ufahamu wake hauwezi kupimika.
6 Yahwe huwainua wanyonge, huwashusha chini wenye jeuri.
7 Mwimbieni Yahwe kwa shukurani, mwimbieni sifa Mungu wetu kwa kinubi.
8 Huzifunika mbingu kwa mawingu na huiandaa mvua kwa ajili ya nchi, akizifanya nyasi kukua juu ya milima.
9 Huwapa wanyama chakula na wana kunguru waliapo.
10 Hapati furaha katika nguvu ya farasi, wala haridhii miguu imara ya mwanadamu.
11 Yahwe huridhia katika wale wanao muheshimu yeye, watumainio katika uaminifu wa agano lake.
12 Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni.
13 Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako.
14 Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora.
15 Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana.
16 Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.
17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo, ni nani awezaye kuhimili baridi aitumayo?
18 Hutuma amri zake na kuziyeyusha, huvumisha upepo wake na hutiririsha maji.
19 Hutangaza neno lake kwa Yakobo, amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
20 Hajafanya hivyo kwa taifa linginelo lolote, na kama ilivyo amri zake, hawazijui. Msifuni Yahwe.