15
1 Zaburi ya Daudi. Yahwe, ni nani atabaki hemani mwako? Ni nani atakaye ishi kwenye mlima wako mtakatifu?
2 Yeyote anaye tembea bila lawama, yeye hufanya kilicho haki na huongea ukweli kutoka moyoni mwake.
3 Yeye huwa hakashfu kwa ulimi wake, hawadhuru wengine, na hamtusi jirani yake.
4 Mtu asiye na maana hudharauliwa machoni pake, bali yeye huwaheshimu wale wanao mhofu Yahwe. Yeye huapa kwa hasara yake mwenyewe na habadilishi ahadi yake.
5 Yeye habadilishi nia yake aazimapo fedha. Yeye hachukui rushwa ili kumshuhudia kinyume asiye na hatia. Yeye afanyanyaye mbambo haya hatatikisika kamwe.