17
1 Maombi ya Daudi. Sikia ombi langu kwa ajili ya haki, Yawhe; uusikilize mwito wangu wa msaada. Uyasikilize maombi yangu yatokayo katika midomo isiyo na udanganyifu.
2 Uthibitisho wangu na uje kutoka uweponi mwako; macho yako na yaone kile kilicho sahihi!
3 Kama utaujaribu moyo wangu, kama utakuja kwangu wakati wa usiku, wewe utanitakasa na hautapata mipango yeyote ya uovu; mdomo wangu hautavunja sheria.
4 Kama kwa matendo ya binadamu, ni katika neno la midomo yako ya kuwa nimejiepusha na njia za wahalifu.
5 Mwenendo wangu umeshikila kwa umakini mwenendo wako; miguu yangu haija teleza.
6 Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea.
7 Onyesha uaminifu wa agano lako katika namna ya ajabu, wewe uokoaye kwa mkono wa haki yako wale wanao kukimbilia wewe kutoka kwa adui zao.
8 Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche katika kivuli cha mbawa zako
9 kutoka katika uwepo wa waovu ambao wananitusi, adui zangu wanizungukao.
10 Wao hawana huruma kwa yeyote; midomo yao huongea kwa majivuno.
11 Wao wame zizunguka hatua zangu. Wamekaza macho yao wanishambulie mpaka ardhini.
12 Wao ni kama mfano wa hasira ya simba mawindoni. Ni kama simba kijana anapotokea mafichoni.
13 Inuka, Yahwe! Uwashambulie! Uwaangushe chini kwenye nyuso zao! Uyaokoe maisha yangu kutokana na waovu kwa upanga wako!
14 Uniokoe kutoka kwa watu hawa kwa mkono wako, Yahwe, kutoka kwa watu wa dunia hii ambao utajiri wao ni maisha haya pekee! Wewe utayajaza matumbo ya wale uwathaminio na utajiri; watakuwa na watoto wengi na wataacha utajiri wao kwa watoto wao.
15 Bali mimi, nitauona uso wako katika haki; Nitashuhudiwa, pale nitakapo amka, na macho yako.