20
1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde
2 na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni.
3 Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa.
4 Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote.
5 Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki.
6 Sasa ninajua ya kuwa Yahwe atawaokoa wapakwa mafuta wake; yeye atamjibu yeye kutoka katika mbingu takatifu kwa uweza wa mkono wake wa kuume ambao waweza kumuokoa yeye.
7 Baadhi hamini katika magari na wengine katika farasi, lakini sisi tumuita Yahwe Mungu wetu.
8 Wao watashushwa chini na kuanguka, bali sisi tutainuka na kusimama wima!
9 Yahwe, umuokoe mfalme; utusaidie sisi tukuitapo.