22
Kwa kiongozi wa muziki; “aina ya muziki wa deer.” Zaburi ya Daudi.
1 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali na wokovu wangu na mbali na maneno yangu yenye uchungu?
2 Mungu wangu, ninalia mchana kutwa, lakini haunijibu, na wakati wa usiku sinyamazi!
3 Bado wewe ni mtakatifu; wewe umekaa kama mfalme pamoja na sifa za Israeli.
4 Mababu zetu walikuamini wewe, na wewe uliwaokoa wao.
5 Walikulilia wewe nao waka okolewa. Wao walikuamini wewe na hawakuvunjwa moyo.
6 Bali mimi ni funza na sio mtu, nisiye faa kwa ubinadamu na hudharauliwa na watu.
7 Wale wote wanionao hunisuta; hunidhihaki; hunitikisia vichwa vyao.
8 Wao husema, “Yeye anamwamini Yahwe; mwache Yahwe amuokoe. Mwache amuokoe yeye, kwa kuwa yeye anampendeza sana Yeye.”
9 Kwa kuwa wewe ulinileta kutoka tumboni; wewe ulinifanya nikuamini wewe wakati nikiwa nanyonya matiti ya mama yangu.
10 Nimekwisha tupwa kwako wewe tokea tumboni; wewe ni Mungu wangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu!
11 Usiwe mbali na mimi, kwa kuwa shida ikaribu; hayupo hata mmoja wa kusaidia.
12 Maksai wengi wananizunguka mimi; maksai wenye nguvu ya Bashan wananizunguka mimi.
13 Wao wanafungua midomo yao kwangu kama simba aungurumaye akirarua windo lake.
14 Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.
15 Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
16 Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
17 Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
18 Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
19 Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!
20 Uiokoe roho yangu na upanga, maisha yangu mwenyewe na makucha ya mbwa mwitu.
21 Uniokoe na mdomo wa simba; uniokoe na mapembe ya ng'ombe wa porini.
22 Nami nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kusanyiko la watu nitakusifu wewe.
23 Ninyi mnao mwogopa Yahwe, msifuni yeye! Ninyi nyote kizazi cha Yakobo, muheshimuni yeye! Simameni katika hofu yake, ninyi nyote kizazi cha Israeli!
24 Kwa kuwa haja dharau au kuchukia mateso ya aliye taabishwa; Yahwe hajamficha uso wake yeye; pindi wale walio taabishwa walipo mlilia yeye, yeye alisikia.
25 Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye.
26 Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele.
27 Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako.
28 Kwa kuwa utawala ni wa Yahwe; yeye ni mtawala wa mataifa.
29 Watu wote wa duniani waliofanikiwa wata sherekea na wata abudu; wale wote washukao katika mavumbi watapiga magoti mbele zake, wale ambao hawawezi kulinda maisha yao wenyewe.
30 Kizazi kijacho kitamtumikia yeye; wao watakiambia kizazi kinachofuatia kuhusu Bwana.
31 Wao watakuja na kuzungumza kuhusu haki yake; wao watawaambia watu ambao bado hawaja zaliwa yale ambayo Yahwe ameyafanya!