25
Zaburi ya Daudi.
1 Kwako, Yahwe, nayainua maisha yangu!
2 Mungu wangu, ninaamini katika wewe. Usiniache niaibishwe; usiwaache maadui zangu wafurahie ushindi wao kwangu.
3 Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu!
4 Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako.
5 Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu.
6 Kumbuka, Yahwe, matendo yako ya huruma na uaminifu wa agano lako; kwa kuwa vimekuwapo siku zote.
7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala uasi wangu; Uniweke akilini mwako pamoja na uaminifu wa agano kwa zababu ya uzuri wa wako, Yahwe!
8 Yahwe ni mzuri na mwenye haki; kwa hiyo yeye huwafundisha njia mwenye dhambi.
9 Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.
10 Njia zote za Yahwe ni za upendo wa kudumu na niaminifu kwa wote wanao tunza agano na maagizo ya amri zake.
11 Kwa ajili ya jina lako, Yahwe, unisamehe dhambi zangu, kwa kuwa ni nyingi mno.
12 Ni nani ambaye anamuogopa Yahwe? Bwana atamfundisha yeye katika njia ambayo anapaswa kuichagua.
13 Maisha yake yataenenda katika uzuri; na uzao wake utairithi nchi.
14 Urafiki wa Yahwe ni kwa ajili ya wale wanao mheshimu yeye, naye hulifanya agano lake lijulikane kwao.
15 Siku zote macho yangu yanamtazama Yahwe, kwa kuwa yeye ataifungua miguu yangu kwenye nyavu.
16 Unigeukie mimi na unihurumie; kwa maana niko peke yangu na niliye matesoni.
17 Maumivu ya moyo wangu yameongezeka; uniondoe katika dhiki hii!
18 Tazama mateso yangu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
19 Ona maadui zangu, kwa maana ni wengi; wananichukia kwa chuki ya kikatili.
20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe; usiniache niaibishwe, Kwa kuwa kwako nakimbilia usalama!
21 Uadilifu na unyofu vinihifadhi, kwa kuwa nina kutumainia wewe.
22 Mungu, uiokoe Israeli, na shida yake yote!