37
Zaburi ya Daudi.
1 Usikereshwe na wafanyao maovu; usiwaonee wivu wale watendao yasiyo haki.
2 Kwa kuwa muda mfupi watakauka kama nyasi na kukauka kama vile mimea ya kijani ikaukavyo wakati wa kiangazi.
3 Uwamini Mungu na kufanya yaliyo mema; uishi katika nchi na uongezeke katika imani.
4 Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.
5 Umkabidhi njia zako Yahwe; uamini katika yeye, naye atatenda kwa niaba yako.
6 Yeye ataidhihilisha haki yako kama mchana na usafi wako kama mwangaza wa mchana.
7 Uwe kumya mbele za Yahwe na umsubiri yeye kwa uvumilivu. Usikasirike ikiwa kuna mtu anafanikiwa kwa kile afanyacho, au afanyapo njama za uovu.
8 Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
9 Watendao maovu watafutiliwa mbali, bali wale wamngojao Yahwe watairithi nchi.
10 Katika muda mfupi mtu mwovu atatoweka; wewe utatazama mahali pake, wala hautamuona.
11 Lakini wapole watairithi nchi nao watafurahia katika mafanikio makubwa.
12 Mtu mwovu hupanga njama kinyume na mwenye haki na kumsagia meno.
13 Bwana humcheka, kwa maana anaona siku yake inakuja.
14 Waovu wametoa nje panga zao na wametayarisha pinde zao ili kuwaangamiza wanyonge na wahitaji, na kuwaua wenye haki.
15 Panga zao zitawaua wenyewe, na pinde zao zitavunjika.
16 Ni bora kuwa mwenye haki maskini kuliko tajiri mwenye mali nyingi.
17 Kwa maana mikono ya watu waovu itavunjika, bali Yahwe huwasaidia watu wenye haki.
18 Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha.
20 Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
21 Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
22 Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
23 Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
24 Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake.
25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
26 Wakati wote yeye ni mkarimu na hukopesha, nao watoto wake hufanyika baraka.
27 Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele.
28 Kwa maana Yahwe hupenda haki naye hawaachi wafuasi waaminifu. Wao hutunzwa milele, lakini uzao wa waovu utafutiliwa mabli.
29 Wenye haki watairithi nchi na kuaa huko milele.
30 Mdomo wa mwenye haki huongea hekima na huongeza haki.
31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; miguu yake haitelezi.
32 Mtu mwovu humvizia mwenye haki na kutafuta kumuua.
33 Yahwe hatamuacha yeye kwenye mkono wa mtu mwovu wala kumlaumu atakapohukumiwa.
34 Umngoje Yahwe na uishike njia yake, naye atakuinua uimiliki nchi. Atakapo waondosha waovu wewe utaona.
35 Nimewaona waovu na mtu wa kutisha akienea kama mti wa kijani katika udongo wa asili.
36 Lakini nilipopita tana mara nyingine, hakuwepo pale. nilimtafuta, lakini sikumpata.
37 Uwachunguze watu waadilifu, na uwatambue wenye haki; kuna hatima nzuri kwa ajili ya mtu wa amani.
38 Mwenye dhambi wataharibiwa kabisa; hatima ya mtu mwovu ni kuondoshwa.
39 Wokovu wa haki unatoka kwa Yahwe; yeye huwalinda wao nyakati za shida.
40 Yahwe huwasaidia na kuwaokoa. Yeye huwaokoa dhidi ya watu waovu na kuwanusuru wao kwa sababu wao wamemkimbilia yeye kwa ajili ya usalama.